• HABARI MPYA

  Jumamosi, Agosti 29, 2015

  WEST HAM YAIGONGA NYUNDO ZA KUTOSHA LIVERPOOL ANFIELD, 3-0 NYUMBANI

  LIVERPOOL imegongwa ‘nyundo’ 3-0 na West Ham jioni ya leo katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Anfield.
  Manuel Lanzini alianza kufunga dakika ya tatu, kabla ya Mark Noble kufunga la pili dakika ya 30 na Diafra Sakho kufunga la tatu dakika za majeruhi.
  Wachezaji Philippe Coutinho wa Liverpool na Noble wa West Ham walitolewa kwa kadi nyekundu. Coutinho ambaye alionyeshwa njano ya pili dakika ya 52 ataukosa mchezo dhidi ya mahasimu Manchester United.
  Kikosi cha Liverpool kilikuwa; Mignolet, Clyne, Skrtel, Lovren, Gomez/Ibe dk78, Can/Moreno dk45, Lucas, Milner, Firmino/Ings dk61, Benteke na Coutinho.
  West Ham; Randolph, Tomkins, Reid, Ogbonna, Cresswell, Kouyate, Obiang, Noble, Lanzini/Oxford dk81, Sakho/Cullen dk90 na Payet/Jarvis dk88.
  Wachezaji wa West Ham wakisherehekea ushindi wao wa kwanza Uwanja wa Anfield ndani ya miaka 52 baada ya kuichapa 3-0 Liverpool leo PICHA ZAIDI GONGA HAPA
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: WEST HAM YAIGONGA NYUNDO ZA KUTOSHA LIVERPOOL ANFIELD, 3-0 NYUMBANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top