• HABARI MPYA

  Ijumaa, Agosti 28, 2015

  WILFRIED BONY AUMIA MGUU, ATEMBELEA MAGONGO

  MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Ivory Coast, Wilfried Bony ataikosa mechi ya klabu yake, Manchester City dhidi ya Watford katika Ligi Kuu ya England baada ya kuumia mguu.
  Mpachika mabao huyo aliyesajiliwa kwa Pauni Milioni 28 kutoka Swansea City msimu uliopita ameposti picha katika akaunti yake ya Instagram leo akitembelea magongo na mguu wake umefungwa.
  Na kocha wa Man City, Manuel Pellegrini amethibitisha Bony hatakuwepo uwanjani kesho, lakini atarejea uwanjani wiki itakayofuata baada ya mechi za kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika, akienda kuichezea Ivory Coast Septemba 5. 
  Wilfried Bony ameposti picha akitembelea magongo na mguu wake wa kushoto umegungwa baada ya kuumia PICHA ZAIDI GONGA HAPA
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: WILFRIED BONY AUMIA MGUU, ATEMBELEA MAGONGO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top