• HABARI MPYA

  Jumamosi, Agosti 29, 2015

  BALAA GANI CHELSEA! YAPIGWA NGWALA DARAJANI, YALALA 2-1 KWA CRYSTAL PALACE

  BALAA gani hili. Kocha Mreno Jose Mourinho jioni ya leo hakuamini macho yake baada ya kuchapwa mabao 2-1 na Crystal Palace nyumbani Uwanja wa Stamford Bridge, London katika mchezo wa Ligi Kuu ya England.
  Matokeo hayo yanawafanya mabingwa hao watetezi, Chelsea wazidiwe kwa pointi nane na vinara Manchester City katika msimamo wa Ligi Kuu.
  Bakary Sako alianza kuifungia Crystal Palace dakika ya 65 kabla ya Radamel Falcao kuisawazishia The Blues dakika ya 79 akimalizia krosi ya Pedro- lakini Joel Ward akawafungia wageni bao la ushindi dakika ya 81.
  Kikosi cha Chelsea kilikuwa: Courtois, Ivanovic, Zouma, Cahill, Azpilicueta/Kenedy, Fabregas, Matic/Loftus Cheek, Pedro, Hazard, Willian/Falcao na Diego Costa.
  Crystal Palace; McCarthy, Ward, Dann, Delaney, Souare, Puncheon, Cabaye, McArthur, Zaha/Bolasie, Wickham na Sako.
  Kipa wa Chelsea, Thibaut Courtois akiwa 'hana hamu' baada ya kutunguliwa na Crystal Palace leo PICHA ZAIDI GONGA HAPA
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: BALAA GANI CHELSEA! YAPIGWA NGWALA DARAJANI, YALALA 2-1 KWA CRYSTAL PALACE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top