• HABARI MPYA

  Jumanne, Agosti 25, 2015

  BALOTELLI AREJEA RASMI AC MILAN BAADA YA KUCHEMSHA LIVERPOOL

  Mario Balotelli amerejea AC Milan kwa mkopo leo baada ya kufuzu vipimo vya afya PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  BALOTELLI NA LIGI ALIZOCHEZA 

  Liverpool (2014-15): Mechi 16 bao moja
  AC Milan (2013-14): Mechi 43 mabao 26
  Man City (2010-13):  Mechi 54 mabao 20
  Inter Milan (2006-10): mechi tano mabao mawili
  Jumla ya gharama zake: Pauni Milioni 59 
  MSHAMBULIAJI Mario Balotelli amerejea kwa mkopo wa muda mrefu wa msimu AC Milan ya Italia baada ya kushindwa kung'ara Liverpool ya England.
  Mshambuliaji huyo ambaye amekuwa akifanya mazoezi nje ya kikosi cha kwanza Liverpool kwa karibu mwezi wote, alikuwa mjini Milan tangu mwishoni mwa wiki kushughulikia mpango wa kuondoka Anfield.
  Balotelli alipigwa picha akitoka kwenye gari aina ya Audi nyeusi akiwa amevalia Puma nyekundu akiingia katika hospitali kwa vipimo kabla ya kusaini Mkataba. Taarifa ya Milan imesema: "Saa 2:26 asubuhi hii, Mario Balotelli amewasili zahanati ya La Madonnina kufanyiwa vipimo vya afya,".
  Balotelli, aliyekuwa analipwa Pauni 80,000 kwa wiki Liverpool, alifunga bao moja tu Ligi Kuu ya England katika ushindi wa 3-2 dhidi ya Tottenham Februari - na mengine matatu katika mashindano ya vikombe. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: BALOTELLI AREJEA RASMI AC MILAN BAADA YA KUCHEMSHA LIVERPOOL Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top