• HABARI MPYA

  Jumamosi, Agosti 29, 2015

  RAHEEM STERLING AING’ARISHA MAN CITY, APIGA BAO IKISHINDA 2-0 LIGI KUU ENGLAND

  MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa England, Raheem Sterling amefunga bao kake la kwanza Manchetser City tangu asajiliwe kwa Pauni Milioni 49, timu hiyo ikishinda 2-0 dhidi ya Watford katika Ligi Kuu ya England jioni ya leo Uwanja wa Etihad.
  Raheem Sterling aliyetokea Liverpool, alifunga bao lake hilo dakika ya 47 akimalizia krosi nzuri ya beki Mfaransa, Bacary Sagna.
  City ilipata bao la pili dakika 10 baadaye kupitia kwa Fernandinho aliyemalizia pasi maridadi ya kiungo wa Hispania, David Silva.
  Kikosi cha Manchester City kilikuwa; Hart, Sagna, Mangala, Kompany, Kolarov, Fernandinho, Toure, Sterling/Iheancho dk90, Silva/Delph dk75, Navas/Nasri dk45 na Aguero.
  Watford; Gomes, Nyom, Prodl, Catchcart, Holebas, Behrami, Capoue/Watson dk76, Abdi/Anya dk63, Ighalo/Layun dk72, Jurado na Deeney.
  Mshambuliaji wa zamani wa Liverpool, Raheem Sterling akimrukia mgongoni Yaya Toure na wachezaji wenzake kushangilia bao lake katika ushindi wa Man City wa 2-0 dhidi ya Watford leo PICHA ZAIDI GONGA HAPA
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: RAHEEM STERLING AING’ARISHA MAN CITY, APIGA BAO IKISHINDA 2-0 LIGI KUU ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top