• HABARI MPYA

  Alhamisi, Agosti 27, 2015

  YANGA SC KUWEKA KAMBI ZANZIBAR KUJIANDAA NA LIGI KUU


  Wachezaji wa Yanga SC wakisherehekea na Ngao ya Jamii wiki iliyopita baada ya kuifunga Azam FC kwa penalti 8-7 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam

  RATIBA YA LIGI KUU YA VODACOM TZ BARA 

  Septemba 12, 2015
  Ndanda FC Vs Mgambo JKT
  African Sports Vs Simba SC
  Majimaji FC Vs JKT Ruvu
  Azam FC Vs Prisons
  Stand United Vs Mtibwa Sugar
  Toto Africans Vs Mwadui
  Mbeya City Vs Kagera Sugar
  Septemba 13, 2015
  Yanga SC Vs Coastal Union
  Septemba 16, 2015
  Yanga SC Vs Prisons
  Mgambo JKT Vs Simba SC
  Majimaji FC Vs Kagera Sugar
  Mbeya City Vs JKT Ruvu
  Stand United Vs Azam FC
  Toto Africans Vs Mtibwa Sugar
  Ndanda FC Vs Coastal Union
  Septemba 17, 2015
  Mwadui FC Vs African Sports
  Septemba 19, 2015
  Stand United Vs African Sports
  Mgambo JKT Vs Majimaji FC
  Prisons Vs Mbeya City
  Yanga SC Vs JKT Ruvu
  Septemba 20, 2015
  Mwadui FC Vs Azam FC
  Mtibwa Sugar Vs Ndanda FC
  Simba SC Vs Kagera Sugar
  Coastal Union Vs Toto Africans
  Septemba 26, 2015
  Simba SC Vs Yanga SC
  Coastal Union Vs Mwadui FC
  Prisons Vs Mgambo JKT
  JKT Ruvu Vs Stand United
  Mtibwa Sugar Vs Majimaji FC
  Kagera Sugar Vs Toto Africans
  Septemba 27, 2015
  African Sports Vs Ndanda FC
  Azam FC Vs Mbeya City
  Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
  YANGA SC wanatarajiwa kuweka kambi ya wiki moja visiwani Zanzibar kuanzia Septemba 6, kujiandaa na Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara itakayoanza wiki itakayofuatia.
  Katibu Mkuu wa Yanga SC, Dk. Jonas Tiboroha amesema kwamba kwa sasa kikosi kipo Dar es Salaam kikiendelea na mazoezi chini ya kocha Hans van der Pluijm.
  “Mazoezi yanaendelea Dar es Salaam kwa sasa, kama unavyojua, wachezaji wetu wengi wamekwenda kuzitumikia timu zao za taifa, hivyo waliobaki wanaendelea na mazoezi,”amesema Dk. Tiboroha.
  Mabingwa hao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, watafungua dimba na Coastal Union ya Tanga Septemba 13 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Wiki iliyopita, Yanga SC ilifungua pazia la Ligi Kuu kwa ushindi wa penalti 8-7 dhidi ya Azam FC katika mchezo wa Ngao ya Jamii, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Siku hiyo, kipa Ally Mustafa ‘Barthez’ alipangua penalti mbili za beki raia wa Ivory Coast, Serge Wawa Pascal na mshambuliaji Ame Ali ‘Zungu’, wakati kipa wa Azam FC, Aishi Manula naye alicheza penalti ya Nahodha wa Yanga SC, Nadir Haroub Ali ‘Cannavaro’.
  Penalti za Yanga SC zilifungwa na Haruna Niyonzima, Deus Kaseke, Amissi Tambwe, Andrey Coutinho, Godfrey Mwashiuya, Thabani Kamusoko, Mbuyu Twite na Kelvin Yondan aliyepiga ya mwisho.
  Penalti za Azam FC zilifungwa na Kipre Herman Tchetche, Nahodha John Raphael Bocco, Himid Mao Mkami, Aggrey Morris, Jean Baptiste Mugiraneza, Erasto Nyoni na Shomary Kapombe. 
  Ushindi huo ni sawa na kisasi baada ya Yanga SC kufungwa kwa penalti 5-3 katika Robo Fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame Julai 29, mwaka huu Uwanja wa Taifa, baada ya sare ya 0-0. 
  Ni mara ya tano sasa Yanga SC kutwaa Ngao ya Jamii ikiwa ni rekodi, baada ya kuifunga Simba SC mara mbili, mwaka 2001 mabao 2-1 na 2010 kwa penalti 3-1 baada ya sare ya 0-0 ndani ya dakika ya 90, kabla ya kuifunga Azam FC miaka mitatu mfululizo, 2013 bao 1-0 na 2014 mabao 3-0.
  Inafuatia Simba SC iliyotwaa Ngao mara mbili, mwaka 2011 wakiifunga Yanga SC 2-0 na 2012 wakiifunga Azam FC 3-2, wakati Mtibwa Sugar ni timu nyingine iliyowahi kutwaa Ngao mwaka 2009 ikiifunga 1-0 Yanga SC.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: YANGA SC KUWEKA KAMBI ZANZIBAR KUJIANDAA NA LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top