• HABARI MPYA

  Jumapili, Agosti 23, 2015

  PEDRO AANZA VIZURI ENGLAND, APIGA BAO NA KUSETI MOJA CHELSEA IKIPIGA MTU 3-2 UGENINI

  Pedro akipongezwa na wenzake baada ya bkuifungia Chelsea katika ushindi wa 3-2 leo PICHA ZAIDI GONGA HAPA


  CHELSEA imeanza rasmi mbio za kutetea taji lake la ubingwa wa Ligi Kuu ya England, baada ya kuichapa mabao 3-2 West Bromwich Albion jioni ya leo Uwanja wa The Hawthorns.
  Nahodha John Terry na mchezaji mpya, Pedro aliyesajiliwa kwa Pauni Milioni 21 kutoka Barcelona wote waliaza leo leo The Hawthorns, wakati Saido Berahino alikosekana kikosi cha West Brom kutokana na kuwa mbioni kuhamia Tottenham.
  Beki wa Chelsea, Nemanja Matic aliwapa wapinzani penalti dakika ya 14 tu, lakini kipa Thibaut Courtois akaokoa mchomo wa James Morrison.
  Pedro akaifungia Chelsea bao la kwanza dakika ya 20 kabla ya kumsetia Diego Costa kufunga la pili dakika ya 30- na Morrison akamtungua tena Courtois kuisawazishia West Brom dakika ya 59 kabla ya Cesar Azpilicueta kuifungia Chelsea bao la ushindi dakika ya 42 kwa pasi ya Costa.
  Nahodha Terry akatolewa kwa kadi nyekundu ya dakika ya 53 kwa kumchezea rafu Salomon Rondon.
  Kikosi cha West Bromwich Albion kilikuwa; Myhill, McAuley, Dawson, Olsson, Brunt, Yacob, Fletcher, McManaman/Gnabry dk77, McClean/Lambert dk61, Morrison/Gardner dk88 na Rondon.
  Chelsea; Courtois, Ivanovic, Terry, Zouma, Azpilicueta, Fabregas, Matic, Willian/Cahill dk56, Hazard, Pedro/Mikel dk84 na Costa/Falcao dk77.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: PEDRO AANZA VIZURI ENGLAND, APIGA BAO NA KUSETI MOJA CHELSEA IKIPIGA MTU 3-2 UGENINI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top