• HABARI MPYA

  Jumamosi, Agosti 29, 2015

  MASIKINI MRISHO NGASSA, KOCHA ALIYEMSAJILI FREE STATE ABWAGA MANYANGA

  Kinnah Phiri akimkabidhi Mrisho Ngassa jezi ya FRee State baada ya kusaini Mei mwaka huu akitokea Yanga SC
  KOCHA aliyemsajili Mrisho Ngassa katika klabu ya Free State Stars, Kinnah Phiri amejiuzulu baada ya timu kupoteza mechi tatu mfululizo za mwanzo katika Ligi Kuu ya Afrika Kusini.
  Baada ya kipigo cha 1-0 kutoka kwa Mpumalanga Blac Aces, 4-0 kutoka kwa Kazier Chiefs na 2-1 mbele ya Ajax Cape Town, Phiri ameondoka na nafasi yake anachukua Mjerumani Ernst Middendorp.
  Middendorp ni kocha wa zamani wa Kaizer Chiefs na Bloemfontein Celtic, ambaye alikuwa anafundisha Chippa United msimu uliopita.
  Mjerumani huyo aliwaacha katika mazingira mabaya Chilli Boys baada ya kusimamishwa Machi kufuatia matokeo mabaya kwa timu hiyo ya Port Elizabeth.
  Ngassa alisajiliwa Mei mwaka huu na Free State ya Bethelehem baada ya kocha Phiri kuvutiwa na soka yake akiwa anacheza Yanga SC ya Tanzania. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MASIKINI MRISHO NGASSA, KOCHA ALIYEMSAJILI FREE STATE ABWAGA MANYANGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top