• HABARI MPYA

  Jumapili, Agosti 30, 2015

  BARCELONA YAICHAPA 1-0 MALAGA LA LIGA, MAMBO YA THOMAS VERMAELEN

  MABINGWA watetezi, Barcelona wamepata ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Malaga Uwanja wa Camp Nou katika mchezo wa La Liga.
  Shukrani kwake mfungaji wa bao hilo pekee, beki Mbelgiji Thomas Vermaelen dakika ya 73. Mbelgiji huyo alikuwa nje kwa majeruhi karibu mwaka mzima msimu uliopita baada ya kusajiliwa kutoka Arsenal.
  Luis Suarez, Lionel Messi na Neymar wote walianza katika safu ya ushambuliaji, lakini hakuna kati yao aliyefumga. 
  Kikosi cha Barcelonakilikuwa Bravo; Sergi Roberto, Mascherano, Vermaelen, Alba/Mathieu dk89, Busquets, Rakitic/Rafinha dk64, Iniesta, Messi, Suarez na Neymar/Sandro dk85.
  Malaga; Kameni; Rosales, Angeleri, Weligton/Albentosa dk25, Torres, Horta, Tissone, Recio; Juankar, Amrabat/Charles dk53.
  Beki wa zamani wa Arsenal, Thomas Vermaelen akipongezwa na mwenzake, Jordi Alba baada ya kuifungia bao pekee Barcelona leo PICHA ZAIDI GONGA HAPA
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: BARCELONA YAICHAPA 1-0 MALAGA LA LIGA, MAMBO YA THOMAS VERMAELEN Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top