• HABARI MPYA

  Jumatano, Agosti 19, 2015

  AZAM TV WAMWAGA FEDHA, KOMBE LA FA LARUDI KUANZA NOVEMBA


  Wachezaji wa Yanga SC mwaka 2001 ambao walitwaa Kombe la FA kwa mara ya mwisho kabla ya kupokonywa na JKT Ruvu 2002, mwaka ambao michuano hiyo ilikufa na sasa inafufuka tena 

  ORODHA YA MABINGWA WA KOMBE LA FA: 

  1967 Yanga SC (Dar es Salaam)
  1985 Maji Maji (Songea)   
  1995 Simba SC (Dar es Salaam)
  1996 Sigara (Dar-es-Salaam)
  1997 Tanzania Stars (Dar es Salaam)
  1998 Tanzania Stars (Dar es Salaam)
  1999 Yanga SC (Dar-es-Salaam)
  2000 Mtibwa Sugar
  2001 Yanga SC (Dar-es-Salaam) 
  2002 JKT Ruvu Stars (Pwani)
  Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
  HATIMAYE michuano ya Kombe la FA Tanzania imerudi rasmi, baada ya Bodi ya Ligi kutangaza leo.
  Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Boniphace Wambura Mgoyo amesema kwamba michuano hiyo itaanza Novemba mwaka huu, ikishirikisha timu za Ligi Kuu na madaraja ya chini.
  Habari zaidi kutoka ndani ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ambazo BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE imezipata zimesema kwamba michuano hiyo inarejea kwa udhamini wa Azam TV.
  Michuano ya Kombe la FA imekuwa ikiibuka na ‘kuyeyuka’ tangu mwaka 1967 kabla ya kupotea moja kwa moja mwaka 2002.
  Mara ya mwisho Kombe la FA lilifanyika mwaka 2002 na JKT Ruvu Stars ya Pwani ikaibuka bingwa baada ya kuifunga Baker Rangers ya Magomeni kwenye fainali.
  Bingwa wa kwanza wa Kombe la FA enzi hizo likiitwa Kombe la FAT ilikuwa Yanga SC mwaka 1967, na michuano hiyo haikufanyika tena hadi 1985 Maji Maji ya Songea ilipotwaa Kombe.
  Kombe la FAT likayeyua tena kabla ya kurejea miaka 10 baadaye, 1995 na Simba SC ikatwaa ubingwa kabla ya kupokonywa na Sigara mwaka 1996, ambao nao walilitema kwa Tanzania Stars mwaka 1997 iliyofanikiwa kulitetea 1998 kabla ya kupokonywa na Yanga SC 1999.
  Ubingwa wa FA mwaka 2000 ulikwenda kwa  Mtibwa Sugar, waliopokonywa na Yanga SC mwaka 2001 kabla ya JKT Ruvu kuwa bingwa wa mwisho wa mashindano hayo mwaka 2002.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: AZAM TV WAMWAGA FEDHA, KOMBE LA FA LARUDI KUANZA NOVEMBA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top