• HABARI MPYA

  Jumanne, Agosti 25, 2015

  MAJIMAJI YACHUKUA WAWILI AZAM FC KWA MKOPO

  Omar Wayne (aliyeruka juu) amepelekwa kwa mkopo Majimaji ya Songea
  MAJIMAJI ya Songea mkoani Ruvuma imesajili wachezaji wawili wa Azam FC kwa mkopo wa muda mrefu wa msimu- beki Ismail Gambo ‘Kussi’ na kiungo Omary Wayne.
  Wawili hao matunda ya akademi ya mabingwa hao wa Afrika Mashariki na kati tayari wamesafiri kwenda Songea kujiunga na Majimaji iliyorejea Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu huu.
  Wawili hao wanafanya idadi ya wachezaji watatu ndani ya wiki moja kutolewa kwa mkopo Azam FC, baada ya winga Joseph Kimwaga kupelekwa Simba SC jana.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MAJIMAJI YACHUKUA WAWILI AZAM FC KWA MKOPO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top