• HABARI MPYA

  Jumamosi, Agosti 29, 2015

  SOMOE NG'ITU KATIBU MPYA TWFA, 'AMGARAGAZA VIBAYA' MPINZANI WAKE

  Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
  MWANDISHI wa mwandamizi wa habari za michezo Tanzania, Somoe Ng'tu (pichani) sasa ndiye Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha Soka ya Wanawake Tanzania (TWFA).
  Hiyo inafuatia baada ya Somoe, anyeandikia gazeti la Nipashe, kupata kura 34 dhidi ya 18 za mpinzani wake Dk Cecilia Makafu katika uchaguzi mdogo wa TWFA kuwania nafasi ya Katibu Msaidizi uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Manispaa ya Kinondoni, Dar es Salaam.
  Katika uchaguzi huo, aliyekuwa Katibu Mkuu wa TWFA, Amina Karuma, alichaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa chama hicho, nafasi iliyoachwa wazi na Linna Kessy, baada ya kupata kura 51 za ndiyo dhidi ya 1 ya hapana kati ya kura 52 zilizopigwa.
  Kufuatia kujiuluzu kwa Karuma katika NAFASI ya ukatibu Mkuu, Wajumbe wa mkutano huo wakairidhia Somoe akaimu nafasi hiyo, hadi pale  mkuu utakapofanyika.
  Wengine waliochaguliwa katika uchaguzi huo mdogo,ni Wajumbe wawili wa Kamati ya Utendaji, Debora Mkemwa aliyepata kura 47 na Theresia Mung'ong'o aliyepata kura 45, huku Mwanaheri Kalolo akishindwa baada ya kuambulia kura 11.
  Akizungumza baada ya ushindi huo, Somoe alisema; "Nimefurahi kushinda nafasi hii, ushindi ni kielelezo tosha cha imani ya wajumbe kwangu, sasa ninaamini ni wakati wa kufanya kazi kwa kushirikiana na wenzangu TWFA kuleta maendeleo ya soka ya wanawake,".
  Kwa upande wake, Amina Karuma aliwaomba  wajumbe wa mkutano  huo maalum ambao ni viongozi wa chama cha soka mikoa, kumpa ushirikiano katika kusukuma mbele soka la wanawake.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SOMOE NG'ITU KATIBU MPYA TWFA, 'AMGARAGAZA VIBAYA' MPINZANI WAKE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top