• HABARI MPYA

  Ijumaa, Agosti 28, 2015

  TWIGA STARS KUANZA NA IVORY COAST MICHEZO YA AFRIKA

  TIMU ya Taifa ya Wanawake (Twiga Stars) inayotarajiwa kuondoka nchini mwishoni mwa mwezi Agosti kuelekea nchini Kongo- Brazzaville kwenye Fainali za Michezo ya Afrika (All Africa Games) imepangwa kufungua dimba na timu ya Wanawake ya Ivory Coast Septemba 6, 2105.
  Twiga Stars iliyoweka kambi kisiwani Zanzibar kwa takribani mwezi mmoja sasa, itacheza mchezo wake pili Septemba 9, dhidi ya Nigeria kabla ya kumalizia mchezo wake wa mwisho hatua ya makundi dhidi ya wenyeji Congo-Brazzavile Septemba 12, 2105.
  Jumla ya timu nane za Wanawake kutoka Barania Afrika zinashirki fainali hizo ambazo ni Nchi za Afrika Kusini, Cameroon, Ghana, Misri (wamejitoa) kundi B, na wenyeji Congo-Brazzavile, Ivory Coast, Nigeria na Tanzania kutoka kundi A.
  Timu mbili za juu kutoka kila kundi zitafuzu kwa hatua ya nusu fainali.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: TWIGA STARS KUANZA NA IVORY COAST MICHEZO YA AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top