• HABARI MPYA

  Jumamosi, Agosti 22, 2015

  DIAMOND NA ALI KIBA 'KUMKATIA UTEPE' DK MAGUFULI KESHO JANGWANI

  WANAMUZIKI nyota zaidi Tanzania, Nasibu Abdul ‘Diamond’ na Ali Saleh Kiba wanatarajiwa kupambana shamrashamra za uzinduzi wa kampeni za mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Pombe Magufuli katika viwanja vya Jangwani, Dar es Salaam.
  'Mahasimu' hao wa muziki nchini- watakuwa sehemu ya orodha ya ndefu ya wanamuziki nyota watakaopamba sherehe hizo kesho Jangwani.
  Kitendo cha Ali Kiba na Diamond kupanda jukwaa moja ni nadra kutokea kutokana na upinzani uliopo kati yao, hiyo watu watakaofika kwenye uzinduzi huo watapata burudani ya bure ya aina yake.
  Mbali na kutamba na nyimbo nzuri kwa kila mmoja wao, kumekuwa na upinzani mkali kuhusu msanii mkali wa kutawala jukwaa, hivyo wawili hao wanatarajiwa kutoa burudani ya kiwango cha juu ili kuendelea kuthibitisha ubora wao.
  Magufuli amepata nafasi hiyo baada ya kupita katika mchujo wa watangaza nia zaidi ya 40 waliojitokeza ndani ya CCM. Uchaguzi Mkuu unatarajiwa kufanyika Oktoba 25, mwaka huu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: DIAMOND NA ALI KIBA 'KUMKATIA UTEPE' DK MAGUFULI KESHO JANGWANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top