• HABARI MPYA

  Jumatatu, Agosti 31, 2015

  CHICHARITO AONDOKA KIMOJA MAN UNITED, AHAMISHIA MABAO YAKE BUNDESLIGA

  Javier Hernandez akiwa na Mkurugenzi wa Usajili wa Bayer Leverkusen, Rudi Voller baada ya kukamilisha uhamisho wake leo PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  TIMU ALIZOCHEZEA JAVIER HERNANDEZ

  Guadalajara (2006-10, mechi 80 mabao 29)
  Manchester United (2010-2015 mechi 157 mabao 59
  Real Madrid (2014-15 mkopo mechi 33 mabao 9
  Bayer Leverkusen (2015- ) 
  MSHAMBULIAJI wa Manchester United, Javier Hernandez amekamilisha uhamisho wa Pauni Milioni 12 kwenda kwa vigogo wa Bundesliga, Bayer Leverkusen.
  Hernandez alitua Ujerumani leo mchana baada ya kushindwa kumshawishi kocha Louis van Gaal kumbakiza Old Trafford.
  Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 msimu uliopita alicheza kwa mkopo kwa vigogo wa La Liga, Real Madrid na licha ya tatizo la safu ya ushambuliaji Man United, hakutumiwa timu hiyo ikichapwa mabao 2-1 na Swansea. 
  Mwanasoka huyo wa kimataifa wa Mexico maarufu kwa jina la utani Chicharito aliyekuwa anatakiwa pia na West Ham United, amesaini Mkataba wa miaka mitatu kwa timu ya Ujerumani.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: CHICHARITO AONDOKA KIMOJA MAN UNITED, AHAMISHIA MABAO YAKE BUNDESLIGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top