• HABARI MPYA

  Jumatatu, Agosti 31, 2015

  YANGA SC YASAJILI 24 TU LIGI KUU, COUTINHO NA TINOCCO NDANI

  Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
  KIUNGO Mbrazil Andrey Coutinho ni miongoni mwa wachezaji saba wa kigeni ambao wameombewa usajili na Yanga SC kwa ajili ya msimu mpya.
  Habari ambazo BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE imezipata kutokana ndani ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF)- ni kwamba Yanga SC imewasilisha jumla ya orodha ya wachezaji 24 kwa ajili ya kikosi chake cha kwanza.
  Kati ya hao kuna wageni saba ambao ni Mbuyu Twite wa DRC, Mbrazil Andrey Coutinho, Haruna Niyonzima wa Rwanda, Vincent Bossou wa Togo, Donald Ngoma, Thabani Kamusoko wa Zimbabwe na Amisi Tambwe wa Burundi.
  Kiungo Mbrazil Andrey Coutinho yumo katika orodha ya wachezaji 24 walioombewa usajili Yanga SC

  Wachezaji wazawa Yanga SC ni Benedict Tinocco, Mudathir Khamis, Deogratius Munishi, Ally Mustafa ‘Barthez’, Salum Telela, Oscar Joshua, Kevin Yondani, Mateo Anthony Simon, Juma Abdul, Pato Ngonyani, Malimi Busungu, Godfrey Mwashiuya, Mwinyi Haji Mngwali, Said Juma Makapu, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Deus Kaseke na Simon Msuva.
  Mabingwa hao watetezi wataanza msimu mpya wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwa kumenyana na Coastal Union ya Tanga Septemba 13, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Mechi za mwanzo kabisa za Ligi Kuu zitachezwa Septemba 12, washindi wa pili wa msimu uliopita, Azam FC wakianza na Prisons Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
  Vigogo Simba SC watafungua dimba na African Sports Uwanja wa Mkwakwani, Ndanda FC watamenyana na Mgambo Shooting Mtwara, Majimaji FC watakuwa wenyeji wa JKT Ruvu Songea, Stand United wataikaribisha Mtibwa Sugar Shinyanga, Toto Africans watakuwa wenyeji wa Mwadui Mwanza na Mbeya City wataikaribisha Kagera Sugar.
  Kipa Benedicto Tinocco wakati anasaini Yanga SC Mei mwaka huu

  KIKOSI KAMILI YANGA SC 2015-2016:
  Makipa; Ally Mustafa ‘Barthez’, Benedict Tinocco, Mudathir Khamis na Deogratius Munishi ‘Dida’.
  Mabeki; Juma Abdul, Oscar Joshua, Mwinyi Haji Mngwali, Pato Ngonyani, Kevin Yondan, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Mbuyu Twite, Vincent na Bossou.
  Viungo; Salum Telela, Andrey Coutinho, Haruna Niyonzima, Thabani Kamusoko, Said Juma, Godfrey Mwashiuya, Deus Kaseke na Simon Msuva.
  Washambuliaji; Mateo Anthony Simon, Donald Ngoma, Malimi Busungu na Amisi Tambwe. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: YANGA SC YASAJILI 24 TU LIGI KUU, COUTINHO NA TINOCCO NDANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top