• HABARI MPYA

  Jumanne, Agosti 25, 2015

  SALAMU ZA KWAHERI ZA IVO SIMBA SC, AAMUA KUREJEA ZAKE KENYA, ASEMA…

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  ALIYEKUWA kipa wa Simba SC kwa misimu mmoja nusu uliopita, Ivo Philip Mapunda (pichani kushoto) amesema anarejea Kenya, baada ya kuachwa na klabu hiyo mapema mwezi huu.
  Ivo aliyewahi kudakia pia Yanga SC, amesema hana kinyongo na Simba SC na anaondoka nafsi yake ikiwa safi kwenda kutafuta maisha sehemu nyingine.
  “Nawashukuru mashabiki wa mpira haswa wa Simba kwa kuwa nami kipindi chote, nilipofanya vibaya na nilipowaudhi mlikuwa nami na ndiyo soka ipo hivyo,”amesema.
  Ivo Ameongeza; “Maisha yana changamoto na ndiyo nimezipata kwa sasa Simba baada ya watu fulani kufanya hivyo, ila naamini maisha ni popote na Mungu ndiye kila kitu,”.
  Ivo amesema kwamba anarudi Kenya ambako bado anakubalika na anaamini atapata timu.
  Ivo alijiunga na Simba SC Desemba 2013 akitokea Gor Mahia ya Kenya katika cha mwaka mmoja na nusu wa klabu hiyo ya Msimbazi, ameidakia jumla ya mechi 39 na kufungwa mabao 25, akiiwezesha timu hiyo kutwaa taji moja, Kombe la Mapinduzi.
  Ivo Mapunda akipongezwa na wenzake Januari mwaka huu baada ya kuiwezesha timu hiyo kutwaa Kombe la Mapinduzi Uwanja wa Amaan, Zanzibar

  Zaidi Ivo aliwafurahisha mno wana Simba kwa kulinda vyema lango kwenye mechi dhidi ya mahasimu, Yanga SC na kwa kipindi chake chote Wekundu wa Msimbazi hawajapoteza mechi dhidi ya watani wao hao.
  Alianza na mechi ya Nani Mtani Jembe mwaka juzi, Simba ikishinda 3-1, akadaka mechi ya Ligi Kuu, timu hizo zikitoka sare ya 1-1 kabla ya Desemba mwaka jana kuiongoza tena timu hiyo kushinda mechi ya Nani Jembe 2 mabao 2-0 na mechi yake ya mwisho ya watani kudaka, Wekundu wa Msimbazi walishinda 1-0 katika Ligi Kuu.
  Ivo Mapunda ameondoka Simba SC baada ya mechi 39, akifungwa mabao 25

  REKODI YA IVO MAPUNDA SIMBA SC
  Simba 3-1 Yanga (Nani Mtani Jembe, alifungwa moja Dar)
  Simba SC 1-0 AFC Leopard (Mapinduzi, hakufungwa Zbar)
  Simba SC 0-0 KCC  (Kombe la Mapinduzi)
  Simba SC 2-0 Chuoni (Robo Fainali Kombe la Mapinduzi)
  Simba SC 2-0 URA (Nusu Fainali Kombe la Mapinduzi)
  Simba SC 0-1 KCC (Fainali Kombe la Mapinduzi, alifungwa moja)
  Simba SC 1-0 Rhino Rangers (Ligi Kuu Bara hakufungwa)
  Simba SC 4-0 JKT Oljoro (Ligi Kuu Bara, hakufungwa)
  Simba SC 1-1 Mtibwa Sugar (Ligi Kuu Bara, alifungwa moja)
  Simba SC 0-1 Mgambo JKT (Ligi Kuu Bara, alifungwa moja)
  Simba SC 0-1 Coastal Union (Ligi Kuu, alifungwa moja)
  Simba SC 1-2 Azam FC (Ligi Kuu, alifungwa mbili)
  Simba SC 1-1 Kagera Sugar (Ligi Kuu, alifungwa moja)
  Simba SC 0-1 Ashanti United (Ligi Kuu, alifungwa moja)
  Simba SC 1-1 Yanga SC (Ligi Kuu, alifungwa moja)
  Simba SC 0-3 ZESCO United (Simba Day, alifungwa mbili Dar)
  Simba SC 2-1 Kilimani City (kirafiki Zanzibar, hakufungwa)
  Simba SC 2-0 Mafunzo (kirafiki Zanzibar, hakufungwa )
  Simba SC 5-0 KMKM (Kirarfiki, Zanziabr hakufungwa)
  Simba SC 3-0 Gor Mahia (Kirafiki, Dar es Salaam, hakufungwa)
  Simba SC 0-1 URA (Kirafiki, Dar es Salaam alifungwa moja) 
  Simba SC 2-2 Coastal Union (Ligi Kuu, alifungwa mbili)
  Simba SC 1-0 Ruvu Shooting (Ligi Kuu, hakufungwa)
  Simba SC 2-4 Mtibwa Sugar (Kirafiki Chamazi, alifungwa nne)
  Simba SC 2-0 Yanga SC (Nani Mtani Jembe, hakufungwa)
  Simba SC 3-1 Mwaduni FC (Kirafiki, Taifa alifungwa moja)
  Simba SC 0-1 Kagera Sugar (Ligi Kuu Taifa, alifungwa moja)
  Simba SC 0-0  Mtibwa Sugar (aliingia dakika ya 90 Simba ikashinda penalti 4-3 Fainali Kombe la Mapinduzi)
  Simba SC 2-1 JKT Ruvu (Ligi Kuu, alifungwa moja)
  Simba SC 0-0 Coastal Union (Ligi Kuu, hakufungwa)
  Simba SC 2-0 Polisi Moro (Ligi Kuu, alidaka kipindi cha kwanza akaumia na kutoka bila kufungwa) 
  Simba SC 0-1 Stand United (alifungwa moja)
  Simba SC 5-0 Prisons (Ligi Kuu, hakufungwa)
  Simba SC 1-0 Yanga SC (Ligi Kuu, hakufungwa)
  Simba SC 1-0 Mtibwa Sugar (Ligi Kuu, hakufungwa)
  Simba SC 0-2 Mgambo Shooting (Ligi Kuu, alifungwa moja akatolewa kwa kadi nyekundu kipindi cha pili)
  Simba SC 4-0 Mgambo JKT (Ligi Kuu, hakufungwa)
  Simba SC 3-0 Ndanda FC (Ligi Kuu, hakufungwa)
  Simba SC 2-1 Azam FC (Ligi Kuu, alifungwa moja).
  Ivo Mapunda wakati anasaini Simba SC Desemba mwaka juzi mjini Nairobi
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SALAMU ZA KWAHERI ZA IVO SIMBA SC, AAMUA KUREJEA ZAKE KENYA, ASEMA… Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top