• HABARI MPYA

    Wednesday, July 01, 2026

    GHALIB NA HERSI WAENDA KUMJULIA HALI NA KUMPA POLE PACOME HOSPITALI


    MFADHILI na Mdhamini wa klabu ya Yanga, Bilionea Ghalin Said Mohamed amemtembelea kumjulia hali na kumpa pole kiungo Muivory Coast, Peodoh Pacome Zouzoua aliyeumia jana kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara, dhidi ya wenyeji, JKT Tanzania Uwanja wa Meja Jenerali Charles Isamuhyo, Mbweni, Dar es Salaam.
    Pamoja na Ghalib, viongozi wa Yanga wakiongozwa na Rais, Hersi Ally Said, wachezaji wenzake, na wa klabu nyingine akiwemo Kocha Mkuu wa Azam FC, Jean-Florent Ikwange Ibengé raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) pia wamemtembelea mchezaji huyo kumpa pole na kuomuombea apone mapema.
    Pacome anaweza kuwa nje ya Uwanja kwa muda wiki sizizopungua sita kuangalia hali yake baada ya kuumia goti jana kwenye mchezo huo ambao Yanga SC ilishinda mabao 3-0 na kutwaa ubingw awa ligi hiyo kwa mara ya tano mfululizo.
    Hiyo ni baada ya Pacome kufanyiwa upasuaji usiku wa jana kwenye hospitali ya Aga Khan kufuatia kuumia goti alipogongana na kiungo wa JKT Tanzania, Hassan Wahabi mwishoni mwa kipindi cha kwanza – na kukimbizwa hospitali moja kwa moja.
    Afisa habari wa Yanga, Ally Shaaban Kamwe amesema baada ya wiki hizo atafanyia uchunguzi mwingine ili kujua tena mustakabali wa maumivu yake.



    “Siku ya jana, Pacome alipata jeraha kubwa lililohitaji matibabu ya haraka. Baada ya tathmini iliyofanywa na jopo la madaktari wa Klabu kwa kushirikiana na madaktari wa Hospitali ya Agha Khan, ilikubaliwa afanyiwe upasuaji,” amesema Kamwe na kuongeza.
    “Majira ya saa nane usiku, upasuaji huo ulifanyika na kukamilika kwa mafanikio. Kwa sasa, Pacome atakuwa chini ya uangalizi wa karibu kwa kipindi cha wiki sita, ambapo baada ya hapo tathmini nyingine itafanyika ili kubaini muda atakaohitaji kabla ya kurejea uwanjani,”.
    Uongozi wa JKT Tanzania na mchezaji Hassan Wahabi wamemtembelea Pacome hospitalini kumpa pole baada ya tukio la jana katika mchezo wa kuhitimisha msimu wa Ligi Kuu.


    Next
    This is the most recent post.
    Older Post
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: GHALIB NA HERSI WAENDA KUMJULIA HALI NA KUMPA POLE PACOME HOSPITALI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top