• HABARI MPYA

  Jumapili, Agosti 30, 2015

  MOSLEY AREJEA ULINGONI BAADA YA MIAKA MIWILI NA KUMTWANGA MAYORGA

  BONDIA Shane 'Sugar' Mosley amerejea ulingoni kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2013 na kumshinda kwa Knockout (KO) raundi ya sita mpinzani wake Ricardo Mayorga katika pambano la marudiano baina ya wababe hao jana.
  Hilo linakuwa pambano la 48 kwa bondia huyo mwenye umri wa miaka 43 sasa, Mosley akiwa amepoteza tisa na sare moja moja, 40 yote akishinda kwa KO baada ya kumkalisha chini Mayorga dakika ya pili na sekunde ya 59.
  Hilo linakuwa pambano la tisa kwa Mayoga mwenye umri wa 41 kupoteza baada ya mapambano 31 akitoa sare pia moja likiwemo alilopigwa na Shane tena walipokutana mara ya kwanza miaka saba iliyopita.
  Bondia wa umri wa miaka 43, Shane Mosley (kushoto) amemshinda kwa knockout (KO) raundi ya sita Ricardo Mayorga jana PICHA ZAIDI GONGA HAPA
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MOSLEY AREJEA ULINGONI BAADA YA MIAKA MIWILI NA KUMTWANGA MAYORGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top