• HABARI MPYA

  Jumamosi, Agosti 29, 2015

  ARSENAL YANG’ARA LIGI KUU ENGLAND, YAICHAPA NEWCASTLE 1-0

  BAO la kujifunga la Fabricio Coloccini limeipa Arsenal ushindi wa ugenini Uwanja wa St James' Park dhidi ya Newcastle United katika mchezo wa Ligi Kuu ya England.
  Katika mchezo huo ambao Newcastle walimaliza pungufu baada ya Aleksandar Mitrovic kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 16, Fabricio Coloccini alijfunga baada ya kubabatizwa na mpira uliopigwa na Alex Oxlade-Chamberlain dakika ya 52.
  Kikosi cha Arsenal kilikuwa; Cech, Bellerin, Gabriel, Koscielny, Monreal, Coquelin, Cazorla, Oxlade-Chamberlain/Arteta dk80, Ramsey, Sanchez na Walcott/Giroud dk70.
  Newcastle; Krul, Janmaat, Mbemba, Coloccini, Haidara, Colback, Anita/Perez dk72, Thauvin/de Jong dk87, Wijnaldum, Sissoko/Cisse dk78 na Mitrovic.
  Winga wa Arsenal, Alex-Oxlade Chamberlain akishangilia baada ya mpira aliopiga kumbabatiza mchezaji wa Newcastle, Fabricio Coloccini na kuingia nyavuni kuipati Arsenal ushindi wa 1-0 Uwanja wa St James' Park PICHA ZAIDI GONGA HAPA
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: ARSENAL YANG’ARA LIGI KUU ENGLAND, YAICHAPA NEWCASTLE 1-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top