• HABARI MPYA

  Jumatatu, Agosti 24, 2015

  ETOILE DU SAHEL WATINGA NUSU FAINALI KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA

  ETOILE du Sahel ya Tunisia imetinga Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya sare ya ugenini ya 1-1 dhidi ya Stade Malien mjini Bamako jana.
  ES Sahel iliyoitoa Yanga SC ya Tanzania katika hatua ya 16 Bora kwa jumla ya mabao 2-1 baada ya sare ya 1-1 Dar es Salaam na ushindi wa 1-0 Tunisia, sasa inafikisha pointi 10 baada ya mechi tano sawa na Al Ahly ya Misri ambayo juzi iliifunga Esperance 1-0 nchini Tunisia nayo kujihakikishia kwenda Nusu Fainali kutoka Kundi A. 

  Etoile du Sahel iliiitoa Yanga SC ya Tanzania katika hatua ya 16 Bora kwa jumla ya mabao 2-1 baada ya sare ya 1-1 Dar es Salaam na ushindi wa 1-0 Tunisia

  Katika Kundi B, Zamalek ya Misri nayo imetinga Nusu Fainali baada ya ushindi wa mabao 2-1 ugenini dhidi ya CS Sfaxien nchini Tunisia hivyo kufikisha pointi 12 sawa na Orlando Pirates ya Afrika Kusini, ambayo juzi imeichapa mabao 2-0 
  AC Leopards ya Kongo.
  Mechi za makundi zitahitimishwa Septemba 12 kwa Zamalek kuikaribisha Orlando Pirates, AC Leopards kuikaribisha CS Sfaxien, Al Ahly kuwa wenyeji wa Stade Malien na ES Sahel kumenyana na ndugu zao, Esperance nchini Tunisia.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: ETOILE DU SAHEL WATINGA NUSU FAINALI KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top