• HABARI MPYA

  Alhamisi, Agosti 27, 2015

  ROONEY APIGA HAT TRICK MAN UNITED YAUA 4-0 NA KUFUZU MAKUNDI LIGI YA MABINGWA ULAYA

  TIMU ya Manchester United imeibuka na ushindi wa ugenini wa mabao 4-0 dhidi ya Bruges katika mechi ya mchujo kuwania kucheza hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. 
  United sasa inafuzu hatua ya makundi kwa ushindi wa jumla wa 7-1 baada ya awali kushinda 3-1 nyumbani.
  Nahodha Wayne Rooney alifunga mabao matatau katika dakika ya 20, 49 na 57, wakati bao lingine la Mashetani hao Wekundu lilifungwa na Ander Herrera.
  United ingeweza kuondoka ushindi mnono zaidi kama Javier Hernandez ‘Chicharito’ asingekosa penalty kipindi cha pili Uwanja wa Jan Breydel.
  Kikosi cha Bruges kilikuwa; Bolat, De Fauw, Castelletto, Duarte, De Bock, Claudemir, Vormer, Vazquez/Vanaken dk62, Bolingoli Mbombo/Cools dk76, De Sutter, Diaby/Dierckx dk63.
  Manchester United; Romero, Darmian, Smalling, Blind, Shaw, Carrick, Herrera/Hernandez dk64, Mata/Young dk62, Schweinsteiger dk46.
  Wayne Rooney akishangilia baada ya kufunga bao la tatu katika ushindi wa 4-0 dhidi ya Bruges usiku huu PICHA ZAIDI GONGA HAPA
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: ROONEY APIGA HAT TRICK MAN UNITED YAUA 4-0 NA KUFUZU MAKUNDI LIGI YA MABINGWA ULAYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top