• HABARI MPYA

  Jumanne, Agosti 25, 2015

  MWADUI KUIONJESHA MAKALI YAKE YA AZAM FC KESHO CHAMAZI

  MABINGWA wa Afrika Mashariki na Kati, Azam FC kesho usiku watamenyana na wageni wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Mwadui FC ya Shinyanga katika mchezo wa kirafiki utakaofanyika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
  Mechi hiyo itakayoonyeshwa moja kwa na Televisheni ya Azam, itaanza Saa 1:00 usiku na Mwadui FC inatarajiwa kuwa kipimo kizuri kwao baada ya jana kutoka sare ya 0-0 na Simba SC Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Kocha Mkuu wa Azam FC, Muingereza Stewart Hall amesema katika mchezo huo atapata fursa ya kuwajaribu wachezaji wake ambao hawana nafasi kikosi cha kwanza kutokana na wachezaji wake kadhaa kwenda kuchezea timu zao za taifa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MWADUI KUIONJESHA MAKALI YAKE YA AZAM FC KESHO CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top