• HABARI MPYA

  Ijumaa, Agosti 21, 2015

  MKWASA ATEUA 22 SAFARI YA TAIFA STARS UTURUKI

  Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa ametaja wachezaji 22 watakaosafiri usiku wa jumapili kuelekea nchini Uturuki kwa kambi

  KOCHA mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro, Charles Boniface Mkwasa ametoa orodha ya wachezaji 22 watakaosafiri usiku wa jumapili kuelekea nchini Uturuki kwa kambi ya wiki moja kujiandaa na mchezo dhidi ya Nigeria Septemba 05, 2015.
  Orodha hiyo ya wachezaji 22 imetoka katika kikosi kilichotangazwa wiki mbili zilizopita na kocha mkuu wa Taifa Stars, ambapo walipata nafasi ya kufanya mazoezi kwa takribani wiki moja katika uwanja wa Karume.
  Wachezaji wote waliochaguliwa kujiunga na timu ya Taifa wanapaswa kuripoti kambini Tansoma Hoteli siku ya jumapili saa 5 asubuhi kwa maandalizi ya mwisho ya safari hiyo.
  Wachezaji waliochaguliwa ni Ally Mustafa ‘Barthez’ (Yanga SC), Aishi Manula (Azam FC), Said Mohamed (Mtibwa Sugar), walinzi Shomari Kapombe (Azam FC), Abdi Banda, Mohamed Hussein, Hassan Isihaka (Simba SC), Juma Abdul, Haji Mngwali, Kelvin Yondani, Nadir Haroub (Yanga SC).
  Viungo Mudathir Yahya, Himid Mao, Frank Domayo (Azam FC), Salum Telela, Deus Kaseke (Yanga SC), Said Ndemla (Simba SC), Washambuliaji John Bocco, Farid Mussa, (Azam FC), Rashid Mandawa (Mwadui FC), Simon Msuva (Yanga SC), na Ibrahim Hajib (Simba SC).
  Taifa Stars inatarajiwa kuondoka jumapili usiku kwa usafiri wa shirika la ndege la Uturuki (Turkish Airlines), na kufika jumatatu asubuhi jijini Istambul, ambapo timu itaelekea katika mji wa Kocael ambapo itaweka kambi ya wiki moja katika hoteli ya Green Park Kartepe.
  Wakati huo huo: Timu ya Taifa ya Wanawake ya Kenya (Harambee Starlets) tayari imewasili kisiwani Zanzibar ikiwa na kikosi cha wachezaji 17 pamoja na viongozi 9 tayari kwa mchezo wa kirafiki dhidi ya Twiga Stars siku ya jumapili.
  Mchezo huo wa kirafiki unatarajiwa kuanza majira ya saa 10 kamili jioni katika Uwanja wa Amani kisiwani Zanzibar, ambapo viingilio vya mchezo huo itakua ni shilingi elfu mbili kwa jukwaa kuu, na shilingi elfu moja kwa mzunguko.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MKWASA ATEUA 22 SAFARI YA TAIFA STARS UTURUKI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top