• HABARI MPYA

  Alhamisi, Agosti 27, 2015

  MRISHO NGASSA MAMBO MAGUMU AFRIKA KUSINI

  KIUNGO mshambuliaji wa Tanzania, Mrisho Khalfan Ngassa jana amecheza kwa dakika 70 timu yake, Free State Stars ikipoteza mechi ya tatu mfululizo dhidi ya Ajax Cape Town katika Ligi Kuu ya ABSA Afrika Kusini.
  Mabao ya Mosa Lebusa dakika ya 30 na Prince Nxumalo dakika ya 40 yalitosha kuizamisha kwa mara ya tatu mfululizo FS Uwanja wa Cape Town.
  Bao la Stars ndilo lilikuwa la kwanza mchezoni dakika ya 26, mfungaji Sthembiso Ngcobo ambaye baadaye alimnyima pasi nzuri Ngassa akiwa nafasi ya kufunga kipindi cha pili.
  Katika mechi mbili zilizotangulia, Free State ilifungwa 1-0 nyumbani Blac Aces kabla ya kuchapwa 4-0 ugenini na Kaizer Chiefs.
  Kikosi cha Ajax Cape Town: Jaakkola, Lolo, Mobara, Coetzee, Lebusa/Jenniker dk74, Mdabuka, Norodien/Gamieldien dk66, Graham, Nxumalo, Losper/Mzwakali dk58 na Cale.
  Free State Stars: Diakite, Masehe, Mashego, Sankara, Tlhone, Da Costa, Kerspuy, Thethani, Obada/Somaeb dk51, Ngasa/Mohomi dk70 na Ngcobo/Masana dk84.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MRISHO NGASSA MAMBO MAGUMU AFRIKA KUSINI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top