• HABARI MPYA

  Ijumaa, Agosti 21, 2015

  VAN PERSIE AENDELEA KUNG'ARA ULAYA, APIGA BAO PEKEE FENERBAHCE YASHINDA 1-0 UGENINI

  MSHAMBULIAJI wa zamani wa Manchester United, Robin van Persie jana ametokea benchi kuifungia bao pekee la ushindi timu yake mpya, Fenerbahce dakika za lala salama katika mchezo wa ugenini wa Europa League dhidi ya Atromitos .
  Nahodha huyo wa zamani wa Arsenal aliyetua Uturuki msimu huu kutoka Manchester United alifunga bao hilo pekee zikiwa zimesalia dakika mbili mchezo kumalizika baada ya kazi nzuri ya mchezaji mwenzake, Caner Erkin.
  Timu ya Uturuki, Fenerbahce ilitawala mchezo huo wa ugenini- maana yake wana matumaini makubwa ya kufanya vyema kwenye mchezo wa marudiano pia na kusonga mbele. 
  Matokeo ya mechi nyingine za mchujo za michuano hiyo ya pili kwa ukubwa kwa ngazi ya klabu Ulaya ni Ajax imeifunga 1-0 Jablonec, Athletic Bilbao imefungwa 3-2 Slovakia na Zilina, Borussia Dortmund imeshinda 4-3 dhidi ya Odds Ballklubb na Southampton imelazimishwa sare ya 1-1 nyumbani na Midtjylland.
  Van Persie akikimbia kushangilia baada ya kuifungia timu yake bao pekee la ushindi nchini Ugiriki usiku wa kuamkia leo PICHA ZAIDI GONGA HAPA
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: VAN PERSIE AENDELEA KUNG'ARA ULAYA, APIGA BAO PEKEE FENERBAHCE YASHINDA 1-0 UGENINI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top