• HABARI MPYA

  Jumamosi, Agosti 22, 2015

  SADIO MANE 'AWATOLEA MBAVUNI' MAN UNITED, AAMUA KUBAKI SOUTHAMPTON

  MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Senegal, Sadio Mane amemuambia kocha Ronald Koeman anataka kubaki Southampton licha ya kutakiwa na Manchester United.
  Kinda huyo wa umri wa miaka 23 anatakiwa na Mashetani Wekundu kwa dau la Pauni Milioni 15, baada ya Man United kuzidiwa kete na Chelsea kwa Pedro aliyetua The Blues kwa dau la Pauni Milioni 21.4 kutoka Barcelona Alhamisi.
  United wapo sokoni kwa sasa wakisaka mshambuliaji na kocha Louis van Gaal amesema ni wao wenyewe walikataa kumnunua Pedro, kwa sababu wanamtaka Mane.
  Sadio Mane has told Ronald Koeman he wants to stay at Southampton despite Manchester United interest PICHA ZAIDI GONGA HAPA
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SADIO MANE 'AWATOLEA MBAVUNI' MAN UNITED, AAMUA KUBAKI SOUTHAMPTON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top