• HABARI MPYA

  Jumatano, Agosti 26, 2015

  AL AHLY WAENDA KUWEKA KAMBI HISPANIA KUJENGA MISULI YA KUINUA 'NDOO YA AFRIKA'

  MABINGWA wa Kombe la Shirikisho Afrika, Al Ahly ya Misri wametangaza ziara ya Hispania kwenda kucheza mchezo wa kirafiki na Getafe CF.
  Al Ahly wanajiandaa mchezo wao wa mwisho wa makundi Kombe la Shirikisho dhidi ya Stade Malien mwezi ujao, Septemba.
  "Timu itaondoka Jumamosi ijayo kwenda Hispania na tutakuwa na kambi fupi kabla ya kucheza mechi ya kirafiki na Getafe CF Septemba 3,"imesema taarifa ya Al Ahly iliyoifikia BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE.
  Mshambuliaji wa Al Ahly, Malick Evouna hatakwenda katika ziara hiyo kwa sababu anaakwenda kujiunga na timu yake ya taifa, Gabon. Al Ahly pia itamkosa mshambuliaji wa Ghana, John Antwi, ambaye atakuwa nje kwa wiki tatu kutokana na kuwa maajeruhi.
  Timu ya Cairo ilifuzu Nusu Fainali za Kombe la Shirikisho kufuatia ushindi wa 1-0 katika mchezo wao uliopita dhidi ya Esperance.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: AL AHLY WAENDA KUWEKA KAMBI HISPANIA KUJENGA MISULI YA KUINUA 'NDOO YA AFRIKA' Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top