• HABARI MPYA

  Jumamosi, Agosti 22, 2015

  SIMBA SC YAMSAJILI KIMWAGA WA AZAM FC KWA MKOPO

  AZAM FC imemtoa kwa mkopo wa muda mrefu wa msimu, winga wake, Joseph Kimwaga (pichani) kwenda klabu ya Simba SC, zote za Dar es Salaam.
  Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba ameiambia BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE kwamba Simba SC iliwasilisha maombi ya kumtaka kwa mkopo Kamwaga na wamekubaliwa.
  "Kwa kuzingatia hali halisi ndani ya klabu kwa sasa tumeona Kimwaga baada ya kupatiwa matibabu mjini Cape Town Afrika ya Kusini na kuwa fiti kabisa, tumruhusu kwenda Simba kwa mkopo,"amesema.
  Kimwaga amekuwa nje ya Uwanja kwa zaidi ya msimu baada ya kuumia goti mwishoni mwa msimu wa 2013-2014 akitoa mchango wa klabu hiyo kubeba ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SIMBA SC YAMSAJILI KIMWAGA WA AZAM FC KWA MKOPO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top