• HABARI MPYA

  Jumanne, Agosti 25, 2015

  HENRY AMUAMBIA WENGER; "NUNUA MSHAMBULIAJI, MECHI MBILI HAKUNA BAO USIOTE UBINGWA"

  NAHODHA wa zamani wa Arsenal, Mfaransa Thierry Henry anaamini klabu hiyo inapaswa kutumia kipindi kilichobaki kabla ya dirisha la usajili kufungwa Septemba 2 kununua kiungo na mshambuliaji.
  The Gunners ililazimishwa sare ya bilakufungana na Liverpool usiku wa jana, licha ya kutawala sana mchezo kipindi cha pili, huku kipa Petr Cech akiokoa michomo miwili ya hatari mno ya Christian Benteke na Philippe Coutinho kipindi cha kwanza.
  Henry anaamini timu yake hiyo ya zamani inahitaji kuongeza makali katika safu yake ya kiungo na ushambuliaji kama wanataka kugombea ubingwa wa Ligi Kuu ya Engand msimu huu, wazo ambalo liliungwa mkono na mchambuzi mwenzake wa Sky Sports, Jamie Carragher.
  Thierry Henry anataka Arsenal isajili kiungo mkabaji au mshambuliaji kabla ya dirisha la usajili kufungwa

  "Nafikiri itakuwa wiki ya aina yake, watanunua mtu mmoja wa mbele au wa katikati ya Uwanja? Waliwakosa wachezaji wengi usiku huu (jana), bado wanahitaji kiungo mkabaji na bado wanahitaji mshambuliaji. Tumekuwa tukisema hivi tangu mwanzoni mwa msimu,"amesema Henry.
  Carragher akaongeza kwamba baada ya Arsenal kushindwa kufunga bao katika mechi zao mbili za kwanza nyumbani, hii ikiwa ni mara ya kwanza tangu mwaka 1979 na sare hiyo inamaanisha timu ya Mfaransa, Arsene Wenger imeshindwa kufunga bao katika mechi zake tano zilizopita za Ligi Kuu ya England nyumbani.
  Olivier Giroud failed to trouble the Liverpool defence on Monday and was substituted after 73 minutes
  Olivier Giroud alishindwa kuisumbua ngome ya Liverpool kabla ya kubadilishwa dakika ya 73 usiku wa Uwanja wa Emirates PICHA ZAIDI GONGA HAPA
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: HENRY AMUAMBIA WENGER; "NUNUA MSHAMBULIAJI, MECHI MBILI HAKUNA BAO USIOTE UBINGWA" Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top