• HABARI MPYA

  Jumapili, Agosti 30, 2015

  BALE, JAMES RODRIGUEZ KILA MMOJA AFUNGA MAWILI REAL MADRID YAANZA LA LIGA KWA 5-0

  MAGALACTICO Real Madrid wameamka na kupata ushindi wa kwanza katika msimu mpya wa La Liga baada ya kuwachapa Real Betis mabao 5-0 Uwanja wa Bernabeu. 
  Gareth Bale alifungua biashara nzuri kwa kufunga bao la kwanza ndani ya dakika mbili, akimalizia krosi ya James Rodriguez, ambaye alifunga bao la pili kwa shuti la mpira wa adhabu dakika ya 39.
  Karim Benzema akafunga bao la tatu dakika mbili baada ya kuanza kipindi cha pili kabla ya mwanasoka wa kimataifa wa Colombia, James kufunga tena dakika moja baadaye.
  Ruben Castro alipata nafasi nzuri ya kuifungia bao la kufutia machozi Betis, lakini mkwaju wake wa penalti ukaokolewa na kipa Keylor Navas dakika ya 62, kabla ya Bale kuhitimisha shangwe za mabao za Real Madrid kwa shuti la umbali wa mita 30. 
  Kikosi cha Real Madrid kilikuwa; Navas, Danilo, Varane, Ramos, Marcelo, Kroos/Casemiro dk64, Modric/Kovacic dk75, James, Bale, Ronaldo na Benzema/Isco dk53.
  Real Betis; Adan, Piccini, Pezzella, Bruno, Molinero/Molina dk45, Torres, N'Diaye/Petros dk81, Cejudo, Vargas, Ceballos/Digard dk53 na Castro.
  Gareth Bale akishangilia baada ya kuifungia Real Madird dakika ya pili PICHA ZAIDI GONGA HAPA
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: BALE, JAMES RODRIGUEZ KILA MMOJA AFUNGA MAWILI REAL MADRID YAANZA LA LIGA KWA 5-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top