• HABARI MPYA

    Monday, August 24, 2015

    MUGIRANEZA NA NIYONZIMA WOTE WAITWA AMAVUBI KUZIVAA DRC NA GHANA AMAHORO

    Jean Baptiste Mugiraneza (kushoto) wa Azam FC na Haruna Hakizimana Niyonzima wa Yanga SC (kulia) wote wameitwa Amavubi

    KOCHA wa timu ya taifa ya Rwanda, Johnny McKinstry amewaita wote viungo Jean Baptiste Mugiraneza 'Migi' wa Azam FC na Haruna Hakizimana Niyonzima 'Fabregas' wa Yanga SC kwa ajili ya michezo miwili kunzia mwishoni mwa wiki.
    Raia huyo wa Ireland Kaskazini ataiongoza Rwanda maarufu kama Amavubi 'Nyigu' Jumamosi wiki hii katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Uwanja wa Amahoro, Kigali na Septemba 5 atakuwa mwenyeji wa Ghana kufuzu Fainali za Mataifa Afrika.
    Kikosi kamili cha Amavubi kinachoingia kambini kesho ni makipa; Olivier Kwizera (APR), Jean Claude Ndoli (APR), Eric Ndayishimiye (Rayon) na Michel Rusheshangoga (APR), mabeki; Fitina Omborenga (Kiyovu), Jean Marie Rukundo (Rayon Sports), Abouba Sibomana (Gor Mahia), Celestin Ndayishimiye (Mukura), Salomon Nirisarike (Saint Truiden), Emery Bayisenge (Lask Linz), Faustin Usengimana (APR) na Ismael Nshutiyamagara (APR).
    Viungo ni Jean Baptiste Mugiraneza (Azam), Djihad Bizimana (APR), Yannick Mukunzi (APR), Imran Nshimiyimana (Police), Haruna Niyonzima (Yanga SC) na washambuliaji Andrew Buteera (APR), Jacques Tuyisenge (Police), Jean Claude Iranzi (APR), Patrick Sibomana (APR), Quentin Rushenguziminega (Lausanne Sport), Isaie Songa (Police), Ernest Sugira (AS Kigali) na Michel Ndahinduka (APR).
    Rwanda na Ghana zinaongoza Kundi H kwa kila timu kuwa na pointi tatu baada ya kushinda mechi zao za kwanza dhidi ya wapinzani wao Msumbiji na Mauritius.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MUGIRANEZA NA NIYONZIMA WOTE WAITWA AMAVUBI KUZIVAA DRC NA GHANA AMAHORO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top