• HABARI MPYA

  Ijumaa, Agosti 28, 2015

  AZAM FC WAENDA MTWARA KUCHEZA NA NDANDA KIRAFIKI KESHO NANGWANDA

  MABINGWA wa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, Azam FC asubuhi hii wanaondoka Dar es Salaam kwenda Mtwara kwa mchezo mmoja wa kirafiki.
  Msemaji wa Azam FC, Jaffar Iddi Maganga ameiambia BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE kwamba timu yao inakwenda Mtwara kwa mwaliko wa Ndanda FC, inayoshiriki LIgi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara pia.
  Amesema Azam FC watakuwa na mechi ya kirafiki dhidi ya Ndanda FC itakayohitimisha shamrashamra za Ndanda Day kesho Uwanja wa Nangwanda Sijaona.

  Jaffar amewataja wachezaji wanaokwenda safari hiyo kuwa ni Metacha Mnatha, Godfrey Elias, Abdallah Heri, Gadiel Michael, Bryson Rafael, Prosper Joseph, David Mwantika, Mcha Khamiss na Kelvin Friday.
  Wengine ni Shaaban Idd, Sadallah Mohamed, Stanislaus Ladislaus, Masoud Abdallah, Optatus Rupekenya, Odas Rajab, Joseph Kauju na benchi la Ufundi, Dennis Kitambi, Iddi Nassor ‘Cheche’, Saleh Jumapili, Twalib Mbarak, John Matambala na Iddi Abubakar.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: AZAM FC WAENDA MTWARA KUCHEZA NA NDANDA KIRAFIKI KESHO NANGWANDA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top