• HABARI MPYA

  Jumamosi, Agosti 29, 2015

  MIDO SHUPAVU LA YANGA SC SAID MAKAPU LANENA; “NIKO KAMILI, TAYARI KWA SHUGHULI”

  Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
  KIUNGO chipukizi wa Yanga SC, Said Juma Makapu amesema kwamba kwa sasa anajiona yuko fiti kabisa kucheza soka ya ushindani na kuisaidia timu yake kutwaa ubingwa.
  “Namshukuru Mungu kwa kweli, kwa sasa nipo fiti kabisa. Na niko tayari kucheza soka ya ushindani na kuisaidia timu yangu kutwaa tena ubingwa,”amesema mchezaji huyo tunda la mradi wa maboresho. 
  Kiungo huyo aliumia mgongo katika mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu uliopita dhidi ya Ndanda FC Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara.
  Said Makapu kulia akiwa na beki Mwinyi Hajji Mngwali baada ya mechi na Azam FC


  Said Makapu akimdhibiti mshambuliaji wa Azam FC, John Bocco 'Adebayor' katika mechi ya Ngao

  Makapu alishindwa kuichezea timu ya taifa katika michuano ya Kombe la COSAFA nchini Afrika Kusini katikati ya mwaka huu na akakosa michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame timu yake ikitolewa Robo Fainali.
  Lakini Makapu alirejea uwanjani baada ya Kombe la Kagame na kucheza mechi zote za kiraiki mjini Mbeya, Yanga ikishinda 4-1 dhidi ya Kemondo, 3-2 dhidi ya Mbeya City na 2-0 dhidi ya Prisons.
  Kocha Hans van der Pluijm akamuanzisha Makapu katika mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Azam FC wiki iliyopita na akaiongoza Yanga SC kushinda kwa penalti 8-7 baada ya sare ya 0-0.
  Kwa Yanga SC, ushindi huo ulikuwa sawa na kulipa kisasi baada ya wao pia kufungwa na Azam FC kwa penalti 3-2 baada ya sare ya 0-0 katika Kombe la Kagame.     
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MIDO SHUPAVU LA YANGA SC SAID MAKAPU LANENA; “NIKO KAMILI, TAYARI KWA SHUGHULI” Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top