• HABARI MPYA

  Jumapili, Agosti 30, 2015

  MANCHESTER CITY YAMWAGA PAUNI MILIONI 52 KUMSAJILI DE BRUYNE

  KLABU ya Manchester City imetangaza kumsajili kiungo wa zamani wa Chelsea, Kevin De Bruyne kutoka Wolfsburg ya Ujerumani kwa dau la Pauni Milioni 52.
  Mbelgiji huyo mwenye umri wa miaka 24, ambaye alicheza kwa miaka miwili Stamford Bridge kabla ya kuhamia Bundesliga mwaka 2014, alifuzu vipimo vya afya jana kuelekea uhamisho huo wa dau kubwa.
  De Bruyne anaingia kwenye orodha ya wachezaji wengine wapya Man City akina Raheem Sterling, Nicolas Otamendi na Fabian Delph.
  Kevin De Bruyne akiwa ameshika jezi ya Manchester City baada ya kukamilisha uhamisho wake Wolfsburg PICHA ZAIDI GONGA HAPA
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MANCHESTER CITY YAMWAGA PAUNI MILIONI 52 KUMSAJILI DE BRUYNE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top