• HABARI MPYA

  Jumapili, Agosti 23, 2015

  YANGA SC NA AZAM FC KATIKA PICHA JANA UWANJA WA TAIFA

  Mshambuliaji wa Yanga SC, Deus Kaseke akipasua katikati ya wachezaji wa Azam FC, beki Serge Wawa na kiungo Farid Mussa katika mchezo wa Ngao ya Jamii jana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Yanga SC ilishinda kwa penalti8-7 baada ya sare ya 0-0 ndani ya dakika 90
  Kiungo wa Azam FC, Farid Mussa akimlamba chenga beki wa Yanga SC, Mbuyu Twite kulia
  Kiungo wa Yanga SC, Haruna Niyonzima akimtoka kiungo wa Azam FC, Jean Baptiste Mugiraneza wote raia wa Rwanda
  Winga wa Yanga SC, Godfrey Mwashiuya akipasua katikati ya wachezaji wa Azam FC, Himid Mao kulia na Ame Ally 'Zungu' kushoto
  Mshambuliaji wa Yanga SC, Donald Ngoma akimiliki mpira mbele ya bekiwa Azam FC, Serge Wawa
  Beki wa Yanga SC, Mwinyi Hajji Mngwali (kulia) akimtoka mshambuliaji wa Azam FC, Kipre Tchetche
  Kipre Tchetche akiwania mpira wa juu dhidi ya beki wa Yanga SC
  Kipa wa Yanga SC, Ally Mustafa 'Barthez' akiokoa mpira dhidi ya KIpr Tchetche wa Azam FC
  Mashabiki wa Yanga SC wakifuatilia mchezo huo jana
  Mgeni rasmi katika mchezo wa jana, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum, Dar es Salaam, Kova (kushoto) akisalimiana na Kocha Msaidizi wa Yanga SC,Charles Boniface Mkwasa katikati ni kocha wa makipa Juma Pondamali  

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: YANGA SC NA AZAM FC KATIKA PICHA JANA UWANJA WA TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top