• HABARI MPYA

  Ijumaa, Agosti 21, 2015

  COASTAL, STAND UNITED NA TOTO AFRICANS ZACHEMSHA USAJILI, FAINI YA TFF INAWAHUSU

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KLABU tatu zimeshindwa kuwasilisha usajili wao wakati dirisha la usajili kwa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom na Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara likifungwa jana.
  Klabu za Coastal Union ya Tanga, Stand United ya Shinyanga na Toto African ya jijini Mwanza zimeshindwa kuwasilisha usajili wao na sasa wanakabiliwa na faini ya Sh. 500,000 kwa kila mchezaji watakapowasiloisha usajili baada ya jana.
  Awali TFF ilitoa muda wa wiki mbili kwa klabu zote nchini kukamilisha usajili, ambapo klabu 13 vya ligi kuu vimeweza kukamilisha ndani ya wakati, klabu 12 vya Daraja la kwanza, klabu 24 za Daraja la pili zimeweza kukamilisha usajili wao ndani ya muda uliopangwa.

  Wakati huo huo: Mchezo wa Ngao ya Jamii kuashiria kufunguliwa kwa pazia la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara utachezwa kesho jumamosi katika uwanja wa Taifasaa 10 kamili jioni, ambapo utazikutanisha timu za Azam FC dhidi ya Yanga zote kutoka jijini Dar es salaam.
  Tiketi za mchezo huo zitaanza kuuzwa kesho asubuhi katika magari maalum maeneo ya uwanja wa Taifa, ambapo kiingilio cha chini kitakua shilingi elfu saba (7,000) na kiingilio cha juu ni shilingi elfu thelathini (30000) kwa VIP A.
  Kuelekea mchezo huo maandalizi yote yamekamilika, ulinzi na usalama utakuwepo wa kutosha, wapenzi na wadau wa mpira wanaombwa kujitokeza kushuhudia mchezo huo. Vimininika, silaha au vitu vinavyoweza kuhatarisha usalama havitaruhusiwa kuingia uwanjani.
  Kabla ya mchezo kati ya Azam FC dhidi ya Yanga SC kutakua na mchezo wa utangulizi utakaozikutanisha timu ya wachezaji wa zamani wa timu ya Taifa (Taifa Stars Legends) dhidi ya Ukonga Veterani.
  Milango ya uwanja wa Taifa itakua wazi kuanzia majira ya saa 5 kamilia asubuhi kutoka nafasi kwa wapenzi wa mpira kuweza kuingia uwanjani mapema.
  Katika hatua nyingine, TFF imetuma salam za rambi rambi kwa chama cha mpira wa miguu mkoa wa Pwani (COREFA) kufuatia kifo cha mwamuzi mstaafu wa mpira miguu Rajabu Zarara kilichotokea juzi usiku jijini Dar es salam.
  Marehemu Zarara licha ya kuwa mwamuzi alikuwa Mjumbe wa Kamati ya Waamuzi mkoa wa Pwani, amezikwa jana jijini Dar es salaam.
  TFF pia imetuma salam za rambi rambi kwa Mwenyekiti wa klabu ya Yanga, kufuatia kifo cha mwanachama wake Athuman Makaranga kilichotokea leo asubuhi jijni Dar es salaam.
  Makaranga alikuwa ni mwanachama wa klabu hiyo miongoni wa wadau wa mpira wa miguu, ambapo alishiriki vyema kwenye michuano ya Kagame iliyomalizika hivi karibuni.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: COASTAL, STAND UNITED NA TOTO AFRICANS ZACHEMSHA USAJILI, FAINI YA TFF INAWAHUSU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top