• HABARI MPYA

  Jumanne, Agosti 25, 2015

  REFA ‘ATIA MFUKONI’ BAO LA ARSENAL YATOKA SARE 0-0 NA LIVERPOOL, PETR CECH AOKOA MAWILI YA WAZI EMIRATES

  ARSENAL wamelazimishwa sare ya bila kufungana na Liverpool Uwanja wa Emirates, London usiku huu katika mchezo wa Ligi Kuu ya England.
  Hata hivyo, Arsenal ilifanikiwa kupata bao lililofungwa na Aaron Ramsey dakika ya tisa, lakini marefa wakalikataa kwa sababu alikuwa ameotea.
  Kipa Petr Cech aliokoa michomo miwili ya hatari ya Christian Benteke na Philippe Coutinho kipindi cha kwanza, huku Olivier Giroud naye akikosa bao la wazi.
  Liverpool wanamaliza mechi ya tatu bila kufungwa bao baada ya kushinda 1-0 mara mbili dhidi ya Stoke City na Bournemouth katika mechi zake mbili za awali za Ligi Kuu.  
  Kikosi cha Arsenal kilikuwa; Cech, Bellerin, Chambers, Gabriel, Monreal, Coquelin/Oxlade-Chamberlain dk82, Ramsey, Ozil, Cazorla, Sanchez na Giroud/Walcott dk73.
  Liverpool; Mignolet, Clyne, Lovren, Skrtel, Gomez, Can, Milner, Lucas/Rossiter dk76, Coutinho/Moreno dk88, Firmino/Ibe dk63 na Benteke.
  Aaron Ramsey akimlalamikia refa msaidizi baada ya kukataa bao alilofunga akidai alikuwa ameotea PICHA ZAIDI GONGA HAPA
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: REFA ‘ATIA MFUKONI’ BAO LA ARSENAL YATOKA SARE 0-0 NA LIVERPOOL, PETR CECH AOKOA MAWILI YA WAZI EMIRATES Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top