• HABARI MPYA

    Thursday, August 20, 2015

    MAN UNITED YAHAMISHIA MAWINDO KWA SADIO MANE BAADA YA KUMKOSA PEDRO

    KLABU ya Manchester United imehamishia mawindo yake kwa mshambuliaji wa Southampton, Sadio Mane baada ya kutoa ofa ya Pauni Milioni 15 kumsajili Msenegali huyo.
    United imelazimika ghafla kuhamia kwa Simba huyo wa Teranga baada ya kuzidiwa kete na mabingwa wa Ligi Kuu ya England, Chelsea katika vita ya saini ya winga wa Barcelona, Pedro.
    Wasaka vipaji wa Mashetani hao Wekundu walikwishaanza kumfuatilia Mane hata kabla hajajiunga na Southampton kama walivyofanya Manchester City na Arsenal.
    Kocha wa Manchester United, Louis van Gaal sasa anataka kumsajili mshambuliaji wa Southampton, Sadio Mane PICHA ZAIDI GONGA HAPA


    Sportsmail's Big Match Stats: Sadio Mane scores quickest PL hat-trick

    Loaded: 0%
    Progress: 0%
    00:00
    Play
    Mute
    Current Time0:00
    /
    Duration Time1:07
    Fullscreen

    WASIFU WA SADIO MANE

    Amecheza mechi 32 za Ligi Kuu ya England akiwa na Southampton na kufunga mabao 10.
    Anashikilia rekodi ya kufunga hat-trick ya haraka zaidi katika Ligi Kuu ya England dhidi ya Aston Villa akitumia dakika 2 na sekunde 56
    Southampton imeiambia Manchester United kwamba Mane hauzwi.
    Chanzo cha habari kutoka Southampton kimesema: "Mane ni tegemeo la timu yetu na tuna mipango naye ya muda mrefu. Hatauzwa,".
    Maofisa wa klabu wamekanusha kwamba ofa imekwishatolewa kwa ajili ya mchezaji huyo na kuistiza kwamba hakuna mawasiliano yaliyofanywa na Manchester United. Lakini BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE inafahamu kwamba mchezaji huyo yuko tayari kuhama na mazungumzo yataanza siku chache zijazo.
    Southampton wanatarajiwa kuoandisha dau la mchezaji huyo hadi Pauni Milioni 25, lakini United wanajiamini watafanikisha dili la kinda huyo wa umri wa miaka 23.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MAN UNITED YAHAMISHIA MAWINDO KWA SADIO MANE BAADA YA KUMKOSA PEDRO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top