• HABARI MPYA

    Sunday, August 23, 2015

    AKINA NGASSA WAFUMULIWA 4-0 NA AKINA TSHABALALA AFRIKA KUSINI

    Siphiwe Tshabalala alipigia msumari wa moto jeneza la Free State jana 

    TIMU ya Free State Stars yenye Mtanzania, Mrisho Khalfan Ngassa imefungwa mabao 4-0 jana na Kaizer Chiefs katika mchezo wa Ligi Kuu ya ABSA Afrika Kusini Uwanja wa FNB, Johannesburg.
    Huo unakuwa mchezo wa pili Free State kufungwa, baada ya wiki mbili zilizopita kufungwa 1-0 nyumbani na Mpumalanga Blac Aces. 
    Katika mchezo wa jana ambao Ngassa hakucheza, mabao ya Kaizer Chiefs yalifungwa na Siboniso Gaxa dakika ya 34, George Lebese dakika ya 42, Chakoroma Liberty aliyejifunga dakika ya 45 na Siphiwe Tshabalala dakika ya 66.
    Kikosi cha Kaizer Chiefs kilikuwa: Khune, Gaxa, Mathoho, Xulu, Masilela, Tshabalala, Letsholonyane, Katsande, Lebese/Maluleka dk73, Parker/Karuru dk80, Mthembu/Ndulula dk66.
    Free State Stars: Mathole, Mashego, Chakoroma, Sankara, Thlone, Venter/Somaeb dk54, Kerspuy, Masehe, Obada/Thetani dk54, Ngcobo/Fileccia dk69 na Mohomi.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AKINA NGASSA WAFUMULIWA 4-0 NA AKINA TSHABALALA AFRIKA KUSINI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top