• HABARI MPYA

  Ijumaa, Agosti 21, 2015

  MKALI MPYA BONGO FLEVA, GALAXY IKANDA APANIA MAKUBWA

  MSANII wa kizazi kipya Galaxy Ikanda, amesema amejipanga kuwa moto wa kuotea mbali katika muziki wa kizazi wa kipya.
  Ikanda alisema amejipanga vizuri kwa ujio 
  wake mpya katika muziki na tayari amesharekodi 
  nyimbo mbili ambazo ana amini zitakuwa tisho.
  Galaxy alisema kwa sasa tayari nyimbo moja ipo hewani na nyimbo ambayo ni ‘Tam Tam’ na kuna wimbo mwingine unaitwa Mzuri tu, unatoka hivi karibuni.

  Alisema ameingia kwenye muziki kwa sababu upo kwenye familia yao, hivyo ajaja kimasihara. "Nimeingia kwenye muziki na nimejipanga kuhakikisha napiga hatua katika kazi yangu"alisema.
  Alisema kuwa licha ya muziki umekuwa na ushindani mkubwa sana kiasi inampelekea msanii makini kuongeza umakini na ubunifu kwenye utendaji.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MKALI MPYA BONGO FLEVA, GALAXY IKANDA APANIA MAKUBWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top