• HABARI MPYA

  Ijumaa, Agosti 21, 2015

  MSIBA YANGA SC, MAKARANGA AFARIKI DUNIA

  MWANACHAMA maarufu wa Yanga SC, Athumani Makaranga (pichani kulia) amefariki dunia asubuhi ya leo baada ya kusumbuliwa na matatizo ya moyo.
  Makaranga amefariki dunia katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam ambako alilazwa jana baada ya kuzidiwa matatizo ya moyo.
  Msiba upo nyumbani kwake Kigogo, Dar es Salaam na klabu ya Yanga SC inatarajiwa kutoa taarifa kamili na ratiba nzima ya mazishi yake.
  Hadi anafariki, Makaranga alikuwa anafanya shughuli za kiusalama ndani ya Yanga na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
  Alikuwepo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kikazi wakati Simba SC ikimenyana na URA katika mchezo wa kirafiki na kushinda 2-1 na taarifa zinasema alizidiwa katikati ya wiki. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MSIBA YANGA SC, MAKARANGA AFARIKI DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top