• HABARI MPYA

    Thursday, August 27, 2015

    MESSI AFUNGUA AKAUNTI YA MABAO AZAM FC IKITOA SARE 1-1 NA MWADUI CHAMAZI

    WINGA Ramadhani Yahya Singano ‘Messi’ usiku huu amefunga bao lake la kwanza Azam FC ikilazimishwa sare ya 1-1 na Mwadui FC ya Shinyanga Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
    Mabingwa hao wa Afrika Mashariki na Kati, walianza kupata bao kupitia kwa Singano ‘Messi’ kabla ya Bakari Kigodeko kuisawazishia Mwadui FC ya kocha Jamhuri Kihwelo ‘Julio’. 
    Hilo linakuwa bao la tatu kwa Azam FC kufungwa kufungwa ndania ya mechi 15 ilizocheza tangu kurejea kwa kocha Muingereza, Stewart John Hall Juni mwaka huu.
    Awali ya hapo, ni Friends Rangers pekee walioweza kuupenya ukuta wa Azam FC ya Stewart na kufunga mara mbili wakilala 4-2 katika mchezo wake wa kwanza kabisa wa kirafiki Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
    Baada ya hapo, Azam FC ilishinda 1-0 dhidi ya JKT Ruvu Chamazi, 1-0 dhidi ya African Sports Tanga, 1-0 dhidi ya Coastal Union Tanga, zote zikiwa mechi za kirafiki kabla ya kuingia Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame na kushinda mechi zote hadi kutwaa ubingwa.
    Ilianza kwa ushindi wa 1-0 dhidi ya KCCA kabla ya kuzifunga 2-0 Malakia ya Sudan Kusini, 5-0 Adama City ya Ethiopia na baadaye kushinda kwa penalti 5-3 dhidi ya Yanga SC baada ya sare ya 0-0 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Katika Nusu Fainali, Azam FC iliichapa tena 1-0 KCCA kabla ya kumaliza kwa ushindi wa 2-0 dhidi ya 2-0 Gor Mahia ya Kenya katika Fainali na kutwaa Kombe la Kagame kwa mara ya kwanza.
    Kutoka hapo, Azam FC ikashinda mechi tatu mfululizo za kirafiki visiwani Zanzibar 1-0 dhidi ya KMKM, 3-0 dhidi ya Mafunzo na 2-0 dhdi ya JKU kabla ya sare ya 0-0 na Yanga SC katika mechi ya Ngao- ambayo mwishowe walifungwa kwa penalti 8-7.
    Kipa wa Azam FC, Aishi Manula alicheza penalti ya kwanza ya Yanga SC iliyopigwa na Nahodha wao, Nadir Haroub Ali ‘Cannavaro’ lakini Serge Wawa akaenda kukosa kabla ya Ame Ally pia kukosa.
    Penalti za Yanga SC zilifungwa na Haruna Niyonzima, Deus Kaseke, Amissi Tambwe, Andrey Coutinho, Godfrey Mwashiuya, Thabani Kamusoko, Mbuyu Twite na Kelvin Yondan aliyepiga ya mwisho.
    Penalti za Azam FC zilifungwa na Kipre Herman Tchetche, Nahodha John Raphael Bocco, Himid Mao Mkami, Aggrey Morris, Jean Baptiste Mugiraneza, Erasto Nyoni na Shomary Kapombe. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MESSI AFUNGUA AKAUNTI YA MABAO AZAM FC IKITOA SARE 1-1 NA MWADUI CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top