• HABARI MPYA

  Jumatano, Agosti 26, 2015

  HISPANIA YAWEKA REKODI MPYA ULAYA, YAINGIZA TIMU TANO MAKUNDI LIGI YA MABINGWA

  HISPANI imeweka rekodi ya kuwa nchi ya kwanza kuingiza timu tano katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya Valencia kuitoa Monaco ya Ufaransa kwa jumla ya mabao 4-3 katika mechi za mchujo usiku wa jana. 
  Los Che, waliokuwa washindi wa pili kwenye michuano hiyo mwaka 2000 na 2001, wanaungana na vinara wengine wa La Liga walioshika nafasi tatu za juu, Barcelona, Real Madrid na Atletico Madrid, wakati Sevilla waliomaliza nafasi ya tano nao pia wamefuzu baada ya kutwaa taji la Europa League mapema mwaka huu.
  Bao la ugenini la mshambuliaji wa zamani wa Manchester City, Alvaro Negredo ndilo lililoibeba Valencia mjini Monacon jana ikifungwa 2-1. Negredo alianza kufunga dakika ya nne kabla ya Andrea Raggi kuwasawazishia wenyeji dakika ya 17 na Elderson Echiejile kufunga la pili dakika ya 75. 
  Mshambuliaji wa zamani wa Manchester City, Alvaro Negredo akishangilia baada ya kuifungia Valencia bao muhimu la ugenini jana dhidi ya Monaco PICHA ZAIDI GONGA HAPA
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: HISPANIA YAWEKA REKODI MPYA ULAYA, YAINGIZA TIMU TANO MAKUNDI LIGI YA MABINGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top