• HABARI MPYA

  Jumamosi, Agosti 29, 2015

  SIMBA SC YACHAPWA 2-0 NA JKU ZANZIBAR, MSENEGALI MPYA ‘AWA MTALII’ UWANJANI

  Na Ameir Khalid, ZANZIBAR
  KOCHA Muingereza, Dylan Kerr amepoteza mchezo wa kwanza, baada ya mechi tisa kufuatia kufungwa mabao 2-0 na JKU Uwanja wa Amaan, Zanzibar katika mchezo wa kirafiki.
  Hii inakuwa mechi ya pili SImba SC inacheza bila kushinda baada ya kulazimishwa sare ya bila kufungana na Mwadui FC ya Shinyanga wiki iliyooita uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuftaia kushinda mechi saba mfululizo awali. 
  Kikosi cha Simba SC kilichofungwa 2-0 na JKU leo Uwanja wa Amaan

  Kerr aliyerithi mikoba ya Mserbia, Goran Kopunovic alianza vizuri Simba SC akishinda mara saba mfululizo 2-1 dhidi ya Zanzibar Kombaini, 4-0 Black Sailor, 2-0 Polisi Zanzibar 3-0 Jang’ombe Boys, 3-2 KMKM zote Uwanja wa Amaan, Zanziabr kabla ya kuzifunga na timu za Uganda, 1-0 SC Villa na 2-1 URA Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam)
  Lakini leo mabao ya Mbarouk Chande dakika ya 32 na na Khamis Said dakika ya 72, yalifuta rekodi yake kutofungwa, huku mshambuliaji aliyekuja kwa majaribio, Msenegali Pape Abdoulaye N’daw akizungumza tu uwanjani bila madhara yoyote.
  Kipa Vincent Angban kutoka Ivory Coast leo aliokota mipira miwili nyavuni kwa mara ya kwanza baada ya mechi saba za kueaka bila kufungwa. 
  Simba SC itashuka tena dimbani kesho kumenyana na Mafunzo Uwanja wa Amaan.
  Simba itashuka dimbani tena leo kwa kupepetana na mabingwa wa soka Zanzibar timu ya Mafunzo.
  Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Angban Vincent, Said Issa, Samir Nuhu, Justuce Majabvi, Awadh Juma, Mwinyi Kazimoto, Simon Sserenkuma/Joseph Kimwaga, Peter Mwanlyanzi/Hamisi Kiiza, Pape Abdoulaye/Mussa Mgosi, Daniel Lyanga, Issa Ngoa.
  JKU; Haji Juma, Suleiman Omar, Abdallah Waziri, Khamis Abdallah, Issa Khaidar, Ismail Khamis, Khamis Said, Ishaka Othman, Amour Omar, Emanuel Martin na Mohammed Abdallah.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SIMBA SC YACHAPWA 2-0 NA JKU ZANZIBAR, MSENEGALI MPYA ‘AWA MTALII’ UWANJANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top