• HABARI MPYA

  Alhamisi, Agosti 20, 2015

  MAN CITY YASAJILI BEKI BORA LA LIGA, SASA NI 'UKUTA WA CHUMA' ETIHAD


  Nicolas Otamendi akiwa ameshika jezi namba 30 aliyokabidhiwa wakati wa kutambulishwa baada ya kukamilisha uhamisho wake wa Pauni Milioni 32 PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  WAPYA WALIOSAJILIWA MAN CITY HADI SASA

  Raheem Sterling (Liverpool, Pauni Milioni 49)
  Fabian Delph (Aston Villa, Pauni Milioni 8)
  Patrick Roberts (Fulham, Pauni Milioni 2, itapanda hadi Milioni 8)
  Enes Unal (Buraspor, Pauni Milioni 2)
  Nicolas Otamendi (Valencia, Pauni Milioni 32)
  Jumla imetumia: Pauni Milioni 99
  KOCHA Manuel Pellegrini ametamba kumnunua 'beki bora' wa La Liga leo baada ya Manchester City kukamilisha uhamisho wa Pauni Milioni 32 wa Nicolas Otamendi kutoka Valencia.
  Mwanasoka huyo wa kimataifa wa Argentina amefaulu vipimo vya afya Jijini Manchester na kukubali Mkataba wa miaka mitano kujiunga na mabingwa hao wa zamani wa Ligi Kuu ya England.
  Otamendi alikuwa anatakiwa pia na Manchester United na Real Madrid, lakini leo ametambulishwa kama mchezaji mpya wa tano wa Man City baada ya Raheem Sterling, Fabian Delph, Enes Unal na Patrick Roberts.
  Inafikiriwa kwamba Valencia wanaweza kutumia fedha za mauzo za mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 kulipia sehemu ya ada ya uhamisho ambayo bado wanadaiwa na City kwa kumnunua mshambuliaji Alvaro Negredo. 
  Otamendi alitajwa katika kikosi bora cha Mwaka cha La Liga msimu uliopita na Pellegrini amesema kwamba klabu yake imepata kifaa cha maana katika wakati mwafaka.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MAN CITY YASAJILI BEKI BORA LA LIGA, SASA NI 'UKUTA WA CHUMA' ETIHAD Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top