// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); MAN UNITED YARUDI MATAWI YA JUU, SASA NI KLABU YA PILI TAJIRI DUNIANI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE MAN UNITED YARUDI MATAWI YA JUU, SASA NI KLABU YA PILI TAJIRI DUNIANI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Thursday, January 22, 2015

    MAN UNITED YARUDI MATAWI YA JUU, SASA NI KLABU YA PILI TAJIRI DUNIANI

    PAMOJA na kuwa msimu mbaya uliopita kwa matokeo ya uwanjani katika Ligi Kuu ya England katika historia yao, lakini Manchester United imeshika nafasi ya pili katika orodha ya klabu tajiri duniani.
    Licha ya kuboronga msimu uliopita hadi kumfukuza kocha David Moyes aliyerithi mikoba ya Sir Alex Ferguson baada ya kumaliza nafasi ya saba katika msimamo wa Ligi Kuu, United inazidiwa na Real Madrid pekee kwa utajiri duniani.
    Timu hiyo ya Old Trafford imeviangusha vigogo vya Ulaya kama Bayern Munich na Barcelona baada ya pato lake kupanda hadi Pauni Milioni 433.2 kutoka Pauni Milioni 363.2.
    Manchester United have moved up to second on the list despite not even being in the Champions League
    Mabingwa wa Ligi Kuu ya England, Manchester City wanabaki kuwa klabu ya pili kwa utajiri duniani kwa klabu za Uingereza, wakishika nafasi ya sita duniani nyuma ya Paris Saint Germain.
    Vinara wa Ligi Kuu England kwa sasa, Chelsea wanabaki nafasi ya saba mbele ya Arsenal iliyo nafasi ya nane. Liverpool, baada ya mafanikio ya msimu uliopita hakuna ajabu wanapanda kutoka nafasi ya 12 hadi ya tisa wakizipita Juventus, Borussia Dortmund na AC Milan.

    KLABU 30 TAJIRI ZAIDI DUNIANI KWA MUJIBU WA RIPOTI YA MAPATO YA MSIMU WA 2013-2014

    1. Real Madrid - £459.5m
    2. Manchester United - £433.2m
    3. Bayern Munich - £407.7m
    4. Barcelona - £405.2m
    5. Paris Saint-Germain - £396.5m
    6. Manchester City - £346.5m
    7. Chelsea - £324.4m
    8. Arsenal - £300.5m
    9. Liverpool - £255.8m
    10. Juventus - £233.6m
    11. Borussia Dortmund - £218.7m
    12. AC Milan - £208.8m
    13. Tottenham - £180.5m
    14. Schalke 04 - £178.9m
    15. Atletico Madrid - £142.1m 
    16. Napoli £137.8m
    17. Inter Milan - £137.1m
    18. Galatasaray - £135.4m
    19. Newcastle United - £129.7m
    20. Everton £120.5m
    21. West Ham United - £105.3m
    22. Aston Villa - £101.9m
    23. Marseille - £100m
    24. Roma - £97.7m
    25. Southampton - £97.3
    26. Benfica - £96.6
    27. Sunderland - £95.7m
    28. Hamburg - £92.2m
    29. Swansea City - £90.5m
    30. Stoke City - £90.1m 


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MAN UNITED YARUDI MATAWI YA JUU, SASA NI KLABU YA PILI TAJIRI DUNIANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top