• HABARI MPYA

  Monday, January 26, 2015

  SAID NDEMLA NJE WIKI MBILI SIMBA SC, NYAMA HIZO!

  Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
  KIUNGO tegemeo wa Simba SC kwa sasa, Said Hamisi Ndemla amepewa mapumziko ya wiki mbili, ilia pate ahueni ya maumivu ya nyama za paja.
  Ndemla aliumia nyama za paja katika Fainali ya Kombe la Mapinduzi wiki mbili zilizopita visiwani Zanzibar, Simba SC ikitwaa taji kwa kuifunga Mtibwa Sugar kwa penalti 4-3 baada ya sare 0-0 dakika 90, lakini ameendelea kucheza na hali hiyo.
  Aliichezea Simba SC ikishinda 2-0 dhidi ya Ndanda FC Uwanja wa Nangwanda Sijaona wiki iliyopita na katikati ya wiki akaichezea timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 23 dhidi ya Rwanda mjini Mwanza, kabla ya jana kurudi katika majukumu ya klabu dhidi ya AzamFC.
  Said Ndemla kulia atapumzishwa kwa wiki mbili ili apate ahueni ya maumivu ya nyama za paja

  Baada ya mchezo wa jana ambao Simba SC ilitoka sare ya 1-1 na Azam FC Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Daktari wa klabu, Yassin Gembe amesema kwamba mchezaji huyo atapewa mapumziko ya wiki mbili.
  “Ndemla atapumzika kwa wiki mbili, kwa sababu ana maumivu ya siku nyingi, ila amekuwa akicheza hivyo hivyo, lakini sasa kuanzia Jumatatu atapumzika kwa wiki mbili,”amesema.
  Hapana shaka mapumziko kwa Ndemla yatatoa fursa kwa kiungo mwingine hodari na chipukizi wa timu hiyo, Abdallah Seseme kuonyesha uwezo wake na kuisaidia timu. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SAID NDEMLA NJE WIKI MBILI SIMBA SC, NYAMA HIZO! Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top