• HABARI MPYA

  Wednesday, January 28, 2015

  IVORY YAPENYA ROBO FAINALI AFCON, CAMEROON NJE, SARAFU KUAMUA NANI APETE KATI YA GUINEA NA MALI

  BAO pekee la Max Gradel dakika ya 35 limeipa Ivory Coast ushindi wa 1-0 katika mchezo wa mwisho wa Kundi D dhidi ya Cameroon na kufuzu Robo Fainali za Kombe la Matifa ya Afrika zinazoendelea Equatorial Guinea.
  Guinea imegawana pointi na Mali kwa sare ya 1-1 katika mchezo mwingine wa Kundi D. Kevin Constant alianza kuifungia Guinea kwa penalti dakika ya 15, kabla ya Modibo Maiga kusawazisha dakika ya 47.
  Ivory Coast inamaliza kileleni mwa kundi hilo kwa pinti zake tano, wakati Mali na Guinea zimemaliza sawa kwa kila kitu hadi wastani wa mabao, na pointi tatu kila mmoja, hivyo sarafu itaamua timu ya kwenda Robo Fainali baina yao. 

  Cameroon imeaga mashindano mapema baada ya mechi za mwisho za makundi leo ikiwa inashika mkia kwa pointi zake mbili, hayo yakiwa matokeo mabaya zaidi kihistoria kwao baada ya miaka.
  Mechi za Robo Fainali zinatarajiwa kuchezwa Jumamosi na Jumapili wiki hii.
  Kongo itamenyana na jirani zao Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Uwanja wa Bata na baadaye wenyeji, Equatorial Guinea watamenyana na Tunisia Jumamosi.
  Jumapili duru la Robo Fainali litafungwa kwa michezo kati ya Mali au Guinea dhidi ya Ghana na 
  Algeria na Ivory Coast Uwanja wa Malabo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: IVORY YAPENYA ROBO FAINALI AFCON, CAMEROON NJE, SARAFU KUAMUA NANI APETE KATI YA GUINEA NA MALI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top