• HABARI MPYA

  Sunday, January 25, 2015

  COUTINHO AOMBA ULINZI WA MAREFA, ASEMA ANAPIGWA ‘KIATU SANA’

  Na Mahmoud Zubeiry, MOROGORO
  KIUNGO Mbrazil wa Yanga SC, Andrey Coutinho ameomba marefa wamlinde, kwa sababu anachezewa rafu sana.
  Akizungumza na BIN ZUBEIRY jana Uwanja wa Jamhuri, Morogoro, Coutinho amesema kwamba anachezewa rafu sana na mabeki wa timu pinzani, na kwa bahati mbaya marefa wamekuwa hawachukui hatua.
  “Kama unachezewa rafu na mchezaji mmoja, na refa hatoi kadi, mchezaji yule yule atarudia kukuchezea rafu tena, na mwingine pia atakuchezea, namna ile ni mbaya. Hakuna mchezaji anayependa kuumia,”alisema.
  Andrey Coutinho akilalamika kwa refa jana Uwanja wa Jamhuri, Morogoro

  Coutinho aliiongoza Yanga SC kushinda bao 1-0 dhidi ya Polisi Uwanja wa Jamhuri, Morogoro katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
  Shukrani kwake, mshambuliaji wa zamani wa Simba SC, Danny Davis Mrwanda aliyefunga bao hilo dakika ya 42 akimalizia mpira uliorudi baada ya kipa Tony Kavishe kupangua krosi ya Simon Msuva.
  Mpira uliozaa bao hilo, ulianzia kwa Sherman ambaye aliangushwa nje kidogo ya boksi na Haruna Niyonzima akaenda kumuanzia haraka Simon Msuva aliyemtoka beki Fanuel Simon na kutia krosi ya bao lililofungwa na Mrwanda, aliyesajiliwa Desemba Yanga SC kutoka Polisi.
  Na Mbrazil huyo amesema ushindi wa jana umewarejeshea hali ya kujiamini, lakini atafurahi kama sasa marefa watakuwa wanawachukulia hatua mabeki wanaowachezea kindava wachezaji wa Yanga.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: COUTINHO AOMBA ULINZI WA MAREFA, ASEMA ANAPIGWA ‘KIATU SANA’ Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top